Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo tarehe 04 Novemba 2020 amekagua maandalizi katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambao utatumika kwa sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho Novemba 05, 2020. Rais Mteule Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuapishwa kesho ili kuanza muhula wa pili wa Serikali ya Awamu ya Tano baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu iliofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi - NEC ilimtangaza kuwa mshindi kwa asilimia 84.4 ya kura zote zilizopigwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwia (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi ,Balozi John Kijazi (kushoto) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo kukagua maandalizi ya uwanja huo utakaotumika kwa shughuli za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa