Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRDADE) imefanya Mkutano wa kuwaunganisha wakulima wa zabibu na taasisi wezeshi katika mnyororo wa thamani,Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ambapo umeshirikisha wakulima wapatao thelathini (30) wa zao la zabibu katika wilaya ya Bahi pamoja na taasisi za kifedha kama vile NBC,NMB nk.Aidha mikutano hiyo imelenga kuendelea kufanyika katika wilaya nyingine kama vile chamwino na dodoma jiji ili kuwaleta pamoja wakulima wa zao la zabibu katika mkoa wa Dodoma.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Bahi Bi.Siwajibu Ally alifungua kutano huo na kuwaomba wakulima kusikiliza kwa makini hoja zitakazotolewa na wadau mbalimbali ili kuboresha zaidi na kuongeza thamani zao la kilimo hicho.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa