Leo, Tarehe 28Julai,2025 Mnamo saa 02:00 asubuhi katika ukumbi wa Hospitali ya Wilaya ya Bahi Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Joachim Thobias Nyingo akiambatana na Bi. Mwanamvua B. Muyongo Katibu Tawala Wilaya ya Bahi amefanya kikao Kazi na Mkurugenzi Mtendajii wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi. Albina William Mtumbuka pamoja na timu ya wataalamu wa Halmashauri (wakuu wa Divisheni na Vitengo) ,Makatibu Tarafa,CHMT na viongozi wa Ulinzi na usalama ambapo katika kikao hicho Wakuu Divisheni na Vitengo waliwasilisha Mipango Kazi Yao kuelekea katika utekelezaji wa bajeti mpya ya Mwaka mpya Wa fedha 2025/26.
Kupitia kikao Kazi hicho Mhe.Nyingo aliwaagiza viongozi hao kuhakikisha Miradi iliyopokea fedha na inayotekelezwa katika Wilaya ya Bahi kusimamiwa kwa ukaribu na kuepuka makosa madogo madogo ya kitaalamu ili iwe na tija kwa Wananchi. Pia,aliwaagiza viongozi wa ngazi zote za Wilaya kuwa na ushirikiano katika kuhudumia Wananchi hasa pale yanapotokea majanga kama uvamizi wa wanyama pori katika vijiji kwani hiyo itarahisisha kupunguza madhali yanayoweza kusababishwa na wanyama hao.
Akienda mbali zaidi kwenye Utoaji huduma za Afya katika ngazi zote amewataka viongozi wa Afya kuhakikisha Wananchi wanapata huduma kama ambavyo muongozo ya Afya anavyoelekeza pamoja kufanya usimamiza WA karibu katika vituo vya Afya,zahanati na hospitali ya Wilaya huduma ziboreshwe ili kupunguza malalamiko kwa Wananchi.
Aidha, katika kikao hicho katibu Tawala wa Wilaya Bi.Mwanamvua B. Muyongo alipata nafasi ya kutoa neno ambapo alihimiza viongozi kuwa karibu na Wananchi wanaowahudumia Kwani Ndio wateja Wao Wa kila siku, hivyo wakiwa na mahusiano nao mzauri katika utoaji hudumahata utendaji Kazi utakuwa Rahisi.
Baada ya kikao hicho kukamilika Mkurugenzi Mtendajii wa ya Wilaya ya Bahi Bi.Albina William Mtumbuka alipokea melekezo na kuahidi kuyafanyia Kazi yeye pamoja na timu yake ya wataalamu pamoja kuahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa taasisi nyingine kwani Ndio umekuwa msingi waendeleo katika Wilaya hiyo.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa