Katika kikao hicho ambacho Mhe.Joachim Nyingo (Mkuu wa Wilaya ya Bahi) alikiongoza kama Mwenyekiti aliwainua Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali ili kujadiri namna ambavyo kupitia idara zao na vitengo walivyojiandaa kutoa huduma za Maendeleo kwa Wananchi kwa kuzingatia thamani ya fedha inayotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Aidha,kupitia kikao hicho Mhe.Nyingo amewataka Viongozi hao kuwa Viongozi mfano na kuwahidumia Wananchi wao kwa Upendo bila kuwabagua kwa Serikali ya Awamu ya sita inaleta Maendeleo kwa wote bila kubagua,kikao hicho kilicho husisha wakuu wa Idara na Vitengo,Watendaji wa Vijiji pamoja na wenyeviti wa Vijiji walisomewa taarifa za fedha zilizopelekwa kwenye maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
Mkuu wa Wilaya pia,aliwataka Viongozi hao kusimamia fedha hizo ili kuhakikisha Maendeleo yanaonekana kwa Wananchi kwani ndio matamanio makubwa ya Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan na ndiyo sababu Mhe.Rais ameruhusu Fedha hizo kutoka mapema na mpaka sasa zimeishapelekewa fedha hizo kwenye akaunti za Taasisi hizo Wilayani Bahi hasa upande wa elimu. Aidha kupitia kikao hicho Mhe.Joachim Nyingo alitumia nafasi hiyo kumtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi.Albina Willium Mtumbuka kwa watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa