Mhe.Waziri wa Mifugo na Uvuvi Ashatu Kijaji hivi leo amefanya ziara yake Wilayani Bahi katika zoezi la Uzinduzi wa chanjo ya Mifugo ikiwemo Ng'ombe,mbuzi,Kondoo na Kuku pamoja na uwasilishwaji wa Mfumo mpya wa utambuzi wa Mifugo ambapo kuanzia sasa mifugo Ikiwemo Ng'ombe watawekewa alama maalumu ya utambuzi yenye namba na yenye kubeba taarifa muhimu za mfugo husika.
Mfumo huu umelenga kuimarisha utambuzi wa haraka wa mifugo na kupunguza wizi ama upotevu holela wa Mifugo. Aidha kupitia zoezi hilo la chanjo takribani Ng'ombe 400 na Mbuzi 200 wamepatiwa chanjo hivi leo na zoezi hilo ni endelevu. Kupitia zoezi hilo Mhe Waziri wa Mifugo na Uvuvi amesisitiza wafugaji kujali afya ya mifugo kwa kujitokeza kwa wingi kuleta mifugo yao kupatiwa chanjo ili kuunga Mkono jitihada kubwa zilizo fanywa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kukisikia kilio cha wafugaji na kuwaletea huduma hiyo ya chanjo ili kuimarisha ustawi wa uchumi kwa wafugaji na afya ya Mifugo ili kufikia viwango vya soko la kimataifa la Mifugo na bidhaa zitokanazo na ufugaji.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa