Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Philip Isdor Mpango ameendelea na ziara zake za kutembelea Wilaya mbalimbali katika mkoa wa Dodoma ambapo safari hii ametembelea Wilaya ya Bahi, ziara hiyo Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango amezindua mradi wa maji katika kata ya Ibihwa pamoja na kugawa N'gombe wa kisasa (Madume ya Mbegu bora) kwa ajili ya kuhamasisha ufugaji wa kisasa Wilaya hiyo.
Aidha, Katika ziara hiyo Mhe. Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano Dkt. Philip Mpango alisikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Wilaya ya Bahi kupitia Mbunge wa Wilaya hiyo Mhe. Keneth Nollo.
Akihutubia Wananchi katika Mkutano wa hadhara Mhe. Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano Dkt. Philip Mpango alioneshwa kufurahishwa Kwa wingi wa watu waliojitokeza kumsikiliza katika mkutano huo pia alipongeza Bahi kufanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la Saba na kasisitiza jitihada zaidi za kuhakikisha watato wanaofaulu wasimamiwa vizuri hadi kufika chuo kikikuu,alipongeza mfuko wa Elimu kulipia wanafunzi sekondari na kusisitiza kwa wanafunzi wa VETA ikiwezekana kama mfuko unatosha waongeze wanafunzi kutoka wanafunzi wa 2 hadi 5 au 10 , na kuzitaka Halmashauri zingine ndani na nje ya mkoa wa Dodoma kuwa na Mfuko wa elimu kama ilivyofanya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.
Pia aliagiza Wizara ya mifugo iangalie zaidi kwenye kuwekeza ufugaji wa samaki bwawa la sulungai ili kuliongezea thamani.
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 687748878
Simu: +255 687748878
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa