Leo Tarehe 29 Julai,2025 Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Joachim Thobias Nyingo akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi. Albina W. Mtumbuka pamoja na Katibu Tawala Wilaya ya Bahi Mwanamvua B. Muyongo wamekutana na wataalamu hao ili kuweza kujadili namna bora ya kuendelea kuboresha utoaji mzurii wa huduma katika sekta ya afya na utatuzi endelevu wa baadhi ya changamoto za huduma za Afya katika Wilaya ya Bahi.
Aidha kupitia kikao hicho Mhe Joachim Thobias Nyingo Mkuu wa Wilaya ya Bahi Amewataka wafawidhi wote kuifanya kazi ya utoaji huduma ya afya kwa wito mkubwa, ufuataji wa kananuni na taratibu zote dhidi ya utoaji huduma.
Aidha Mhe Mkuu wa Wilaya ya Bahi Joachim Thobias Nyingo kupitia kikao hicho ametumia nafasi hiyo kusikiliza kero na changamoto zinazo ikumba Sekta ya afya kupitia Waganga Wafawidhi na kuzitolea ufumbuzi kupitia kikao hicho lengo ikiwa ni kuinua kiwango cha ufanisi wa kiutendaji na kuboresha mtiririko mzuri wa utoaji wa huduma kwa Wananchi wa Wilaya ya Bahi.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa