MIRADI YAZIDI KUMIMINIKA BAHI NA SASA NI “RAIA MAKINI”.
Mradi wa “RAIA MAKINI” ni Mradi unaohusu juhudi za kukuza Ushiriki wa Asasi za Kiraia na Wananchi katika Usimamizi wa Rasilimali za Umma ili kuchochea Maendeleo Endelevu na Ustawi wa Uchumi Nchini Tanzania. Kupitia mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi katika mkoa wa Dodoma (NGONEDO) wenye jukumu la kuratibu, kujenga uwezo na kuimarisha ushirikiano miongoni mwa wanachama wake na wadau wengine katika shughuli za maendeleo.
Na sasa ni katika Wilaya ya Bahi ambapo mradi unatekelezwa na Cross Connect Tanzania (CCT) na Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Dodoma (NGONEDO). Aidha, mradi unatarajia kutekelezwa kwa muda wa miezi 30 sawa na miaka 2 na miezi 5 ukihusisha Vijiji vinne (4) katika Wilaya ya Bahi Ambavyo ni Ibhiwa, Bahi Sokoni, Mpamantwa na Mayamaya.
Mradi huu unatarajiwa kuleta mabadiliko chanya katika usimamizi wa rasilimali na kukuza uwajibikaji wa viongozi kwa kushirikisha jamii kikamilifu katika mifumo ya maamuzi katika wilaya ya Bahi. Akizingumza na viongozi wa Halmashauri, Maafisa wa serikali, na wawakilishi wa jamii leo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mratibu wa NGONEDO Ndugu. Edward Mbogo ametaja Malengo Mahususi ya Mradi wa “Raia Makini” kuwa ni: -
1.Kuzalisha na kusambaza taarifa sahihi na rahisi kueleweka kuhusu usimamizi wa rasilimali za umma ili kuwawezesha wananchi kushiriki mijadala ya umma na kushawishi sera.
2.Kuimarisha uwezo wa wananchi na wadau kudai uwajibikaji kutoka serikalini pamoja na Kukuza ushirikiano kati ya mashirika ya kiraia, vyombo vya habari na wananchi katika mijadala ya kijamii na kushawishi maboresho ya usimamizi wa rasilimali.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa