Mradi huu unatekelezwa katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma na ulianza hatua ya kwanza Julai 2024 ukianza na Wilaya ya Chemba,Kondoa DC na Kondoa TC na uko katika awamu ya pili inayohusisha Wilaya ya Bahi, Dodoma JiJi na Chamwino. Mradi huo unahusisha kuvitambua vikundi na kuviwezesha, kuhuisha uwezo wa vikundi kufikia usawa wa kijinsia na kumuwezesha mwanamke kupitia idara ya Maendeleo ya Jamii.
Vikundi hivyo vitatambuliwa na kujengewa uwezo na kuwezeshwa kifedha ikiwa ni pamoja na kuvipa elimu ya fedha ili viweze kufikia malengo, Mradi huu haulengi kutoa mikopo bali Ruzuku na kusimamia ili ruzuku Ile iweze kuleta tija na kuleta chachu katika kuboresha usawa wa Kijinsia. Akiwasilisha katika menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mkurugenzi wa Mradi huo Ndugu. Nestory Mchanga amesema lengo kuu la mradi huo ni kushiriki katika kutekeleza Sera kwa kuwainua wanawake kiuchumi kuanzia ngazi ya kijamii lakini pia na ukatili wa kijinsia pamoja na Haki na usawa wa kiuchumi jinsia uongozi na uchumi kuanzia ngazi ya Jamii mpaka ngazi ya taifa,jinsia na utawala Bora pamoja na jinsia na Mazingira.
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi Ndugu.Boniface Wilson amewashukuru watu Mradi huo kwa kuona umuhumi kuutambulisha mradi huo kwa menejimenti ya Wilaya ili kuleta tija zaidi katika usimimamizi na ufuatiliaji ili vikundi viinuke na kuleta tija kwa Jamii.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa