Katika ziara ya hiyo Mhe Godwin Gondwe aliwataka wananchi wa vijiji vya Zanka na Mkondai kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kupitia wahisani mbalimbali kujitolea nguvu kazi katika hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo endelevu wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (SRWSS).Katika utekelezaji wa mradi huo Zahanati ya Zanka imepewa Tsh.52,000,000.Shule msingi Zanka imepewa Tsh.48,000,000 na Shule ya msingi Mkondai imepewa Tsh.44,000,000 na kufanya vijiji hivyo viwili kupewa jumla ya Tsh. 144,000,000.
Fedha hizo zinahusisha ujenzi wa miundombinu ya usafi wa mazingira ambayo ni vyoo,maji,vichomea taka,shimo la kutupia kondo la nyuma,shimo la kutupia majivu, uzio pamoja na masinki ya kunawia mikono.
Aidha, wananchi wa vijiji hivyo wameonesha kufurahishwa kwa ujio wa mradi huo na kuahidi kushiriki katika utekelezaji wa hatua za awali za mradi ambazo zimeshaanza kutekelezwa.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa