Na Benton Nollo, Bahi
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda amesema ili jamii iweze kushiriki vema katika shughuli mbalimbali za maendeleo ni lazima iwe na afya njema, ambayo hupatikana kwa mtu kuwa na lishe bora.
Munkunda ameyasema hayo wakati anafunga kikao cha kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 pamoja na taarifa ya Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2020 kilichoketi Bahi tarehe 22 Juni 2020.
Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza Wataalam wa Afya wanaotoa huduma vituoni na Watoa Huduma Ngazi ya Jamii kwa kushirikiana vema na Jukwaa la Lishe Tanzania - PANITA kupitia Mradi wa Lishe Endelevu, wameweza kutekeleza Afua tisa (9) za mkataba huo kwa asilimia 81.7 katika kipindi hicho.
"Suala la lishe katika Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa vipaumbele vyetu kwani tunaamini ili jamii iweze kushiriki vema katika shughuli za kujiletea maendeleo na kukuza uchumi ni lazima iwe na afya njema na Afya njema inatokana na lishe bora". Anasema Munkunda.
Munkunda amesema kuwa hata tarehe 29 Juni 2020 shule zitakapofunguliwa, wilaya imeweka mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni ili waweze kumudu vizuri masomo yao.
Pia, Munkunda ametoa wito kwa akina mama wajawazito kutumia vidonge vya kuongeza damu lakini pia Wataalam wa Afya waendelee kutoa unasihi wa lishe kwa wazazi au walezi wa watoto wenye umri kati ya miezi 0 hadi 23.
Kadhalika, amewasihi kuèndelea kutoa matone ya Vitamini 'A' kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 59.
Munkunda pia, amewahimiza Wataalam hao kuendelea kuwaibua watoto wenye utapiamlo mkali ili waweze kupatiwa matibabu.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Dkt. Philipina Philipo ameushukuru Uongozi wa Jukwaa la Lishe kwa kushirikiana vema na Wilaya ya Bahi kutekeleza maazimio ya Mkataba wa Lishe.
Naye Mkurugenzi wa Mtendaji wa PANITA, Tumaini Mikindo ameupongeza Uongozi wa Wilaya ya Bahi kwa kutekeleza maazimio hayo na ameiomba Halmashauri kuendelea kufanya ukaguzi wa vyakula katika maeneo ya biashara na kutoa fedha kupitia mapato ya ndani kutekeleza shughuli za lishe.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Dkt. Philipina Philipo akizungumza wakati kikao cha kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 pamoja na taarifa ya Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2020 kilichoketi Bahi tarehe 22 Juni 2020.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Lishe Tanzania - PANITA, Tumaini Mikindo akizungumza wakati kikao cha kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 pamoja na taarifa ya Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2020 kilichoketi Bahi tarehe 22 Juni 2020.
Mratibu wa Programu wa Jukwaa la Lishe Tanzania - PANITA, Jane Msagati akizungumza wakati kikao cha kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 pamoja na taarifa ya Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2020 kilichoketi Bahi tarehe 22 Juni 2020.
Wajumbe wa Kamati ya Lishe Wilaya ya Bahi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanahamisi Munkunda (hayupo pichani) wakati akifunga kikao cha kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 pamoja na taarifa ya Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2020 kilichoketi Bahi tarehe 22 Juni 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda (wa pili kushoto waliokaa), Afisa Lishe Mkoa wa Dodoma, Heriet Carin (wa pili kulia waliokaa), Mganga Mkuu Wilaya ya Bahi, Dkt. Philipina Philipo (wa kwanza kulia waliokaa) Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Lishe Tanzania (wa kwanza kushoto waliokaa) na Wajumbe wa Kamati ya Lishe Wilaya ya Bahi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufungwa kwa kikao cha kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 pamoja na taarifa ya Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2020 kilichoketi Bahi tarehe 22 Juni 2020. (Picha zote na Benton Nollo)
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa