Mahakama Kuu ya Gauteng imeamuru kuachiwa kwa ndege ya Serikali ya Tanzania inayosimamiwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) iliyokuwa imezuiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini tangu Agosti 24, 2019.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro amesema nchini humo kuwa, Mahakama hiyo imekubali hoja zote za mawakili wa Tanzania hivyo Serikali imeshinda kesi na ndege imeruhusiwa kuondolewa uwanjani hapo.
Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Mahakama hiyo pia imeamuru mlalamikaji alipe gharama za kesi.
Dkt. Ndumbaro amesema, Mahakama imesema, kama Steyn ana hoja nyingine anaweza kufungua kesi Tanzania, na kwamba, amri ya Mahakama ya Tanzania inaweza ikatekelezwa na Mahakama za Tanzania na si Mahakama za Afrika Kusini.
Amesema, mlalamikaji jana alifungua kesi nyingine kupinga hukumu iliyosomwa leo hivyo wanashangaa alijuaje hukumu hiyo ingekuwa dhidi yake hadi akakata rufaa kabla ya kusomwa hukumu leo.
"Kwa hiyo sisi tunaishukuru sana Mahakama ya Afrika Kusini kwa kutenda haki lakini tunawashukuru zaidi Watanzania ambao wameunga mkono juhudi zetu za kuinasua ndege hii kutoka huku Afrika Kusini" amesema Dkt. Ndumbaro.
Chanzo: tovuti ya habarileo (www.habarileo.co.tz)
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa