Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa ametangaza rasmi tarehe ya kuvunjwa kwa Mabaraza ya Madiwani katika Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini, ikiwa ni hatua ya maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Akitoa Tamko hilo leo Juni 15,2025 jijini Dodoma, Waziri Mchengerwa amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288, kifungu cha 84A, na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287, kifungu cha 178A, amesaini notisi mbili muhimu za kuvunjwa kwa Mabaraza hayo.
"Notisi ya Kuvunjwa kwa Mabaraza ya Madiwani katika Mamlaka za Wilaya, 2025, na ya pili ni Notisi ya Kuvunjwa kwa Mabaraza ya Madiwani katika Mamlaka za Miji, 2025,"
Notisi hizo zinatarajiwa kuchapishwa katika Gazeti la Serikali hivi karibuni, na zinabainisha kuwa vikao vyote vya Halmashauri pamoja na Kamati zake lazima vikome kufikia tarehe 20 Juni, 2025 — siku saba kabla ya kuvunjwa rasmi kwa Bunge.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa