Leo tarehe 08/07/2025, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetoa mafunzo ya siku moja kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kufanya tathimini katika Mfumo wa (E-Utendaji) baada ya kupandisha Mipango kazi yao na kuithibisha katika Mfumo wa (E-Utendaji) maarufu kama PEPMIS.
Mafunzo hayo ambayo yalihusisha Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja, Wakuu wa Divisheni,Waratibu elimu Kata,Walimu Wakuu,Watendaji wa Kata, na Waganga Wafawidhi. Akiongoza mafunzo hayo Ndugu. David Wembe amewasihi watumishi kuwafanya tathmini kwa kuzingatia sharia taratibu na miongozo ya utumishi wa Umma.
Aidha,mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Side-View Wilayani hapo na kuhudhuliwa na jumla ya Watumishi 216 na changamoto mbali mbali za uelewa juu matumizi mbalimbali ya mfumo na changamoto zake viliwezwa kutatuliwa.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa