Na Benton Nollo, Bahi
Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya ya Bahi, Awadhi Mashombo amelieleza Baraza la Madiwani kuwa Wakulima wote wa zao la Ufuta wilayani humo kuanzia mwaka huu (2020) sasa watauza zao hilo kwa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani ili zao hilo liwe na tija kwao.
Mashombo ameyasema hayo wakati akijibu swali lililoulizwa na Diwani wa Kata ya Babayu, Hussein Kamau kwenye kikao cha Baraza la Madiwani robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2019/2020 aliyehitaji kujua utaratibu mpya wa kuuza zao hilo baada ya kuulizwa na wananchi wake kwa njia ya simu kwamba wanaona kuwa utaratibu umebadilika.
Kupitia kikao hicho kilichoketi tarehe 30 Aprili 2020 kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Bahi, Mashombo amesema kuwa mauzo ya ufuta yatasimamiwa na Chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Balalu - BALALU AMCOS.
Ambapo ameeleza kwamba ufuta utakusanywa katika vituo mbalimbali vitakavyowekwa na BALALU AMCOS katika Kata na Vijiji mbalimbali. Hivyo, wafanyabiashara wote Bahi hawataruhusiwa kukusanya au kununua ufuta kwa mkulima isipokuwa kwa BALALU AMCOS ambaye ameidhinishwa na Halmashauri.
Mashombo amelieleza Baraza kuwa mfumo huo unaanza kutekelezwa baada ya kupokea maelekezo yalitotolewa na Wizara ya Kilimo, Umwagiliji na Ushirika kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara ambazo zimerasmisha zao hilo kuuzwa kwa mfumo huo.
“Kwa kuwa Wilaya yetu ina Chama cha Ushirika kimoja ambacho ni BALALU AMCOS basi kwa kushirikiana na Maafisa Ugani waliopo kwenye Kata zote, ndicho kitakachokusanya ufuta kutoka kwa wakulima na kuupeleka katika ghala ambako mnada ndiko utakakokuwa unafanyika”. Anasema Mashombo na kuongeza;
“Hivyo, ununuzi utakuwa unafanyika kwa njia ya mnada na ununuzi huo utakuwa wa ushindani kwa hiyo bei itakuwa ya mnada na siyo bei za wachuuzi ambao kila mmoja anaenda kununua kwa mkulima mmoja mmoja…wakulima watalipwa baada ya mnadakufanyika na watalipwa kupitia Benki”. Amesema Mashombo.
Mashombo amesema kuwa ili kupambana na wakulima wasio halisi (Kangomba), tayari Halmashauri kupitia Idara hiyo imeshawapatia maelekezo Maafisa Ugani kuwatambua wakulima wote ambao wamelima zao la ufuta kwa msimu huu na siku ya kuuza atakayekuja na mzigo ndiye atakayetambuliwa.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakiwa katika kikao cha tatu cha Baraza hilo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Bahi tarehe 30 Aprili 2020.
Katibu wa Baraza la Madiwani ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga akizungumza wakati wa kikao cha tatu cha Baraza hilo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Bahi tarehe 30 Aprili 2020. Ambapo pamoja na kuwasilishwa kwa taarifa za utekelezaji wa Jamati za Kudumu za Halmashauri pia iliwasilishwa taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kipindi hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akizungumza wakati wa kikao cha tatu cha Baraza la Madiwani kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Bahi tarehe 30 Aprili 2020.
Afisa Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma, Nathalis Linuma akizungumza wakati wa kikao cha tatu cha Baraza la Madiwani kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Bahi tarehe 30 Aprili 2020.
Baadhi ya Madiwani wakizungumza wakati wa kikao cha tatu cha Baraza la Madiwani kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Bahi tarehe 30 Aprili 2020.
Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Bahi, Helen Mselemu akijitambulisha mbele ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani na Viongozi waliohudhuria kikao cha tatu cha Baraza hilo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 tarehe 30 Aprili 2020. Mselemu amehamia wilayani humo akitokea Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI).
Afisa Ardhi na Maliasili Wilaya ya Bahi, Utongani akijitambulisha mbele ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani na Viongozi waliohudhuria kikao cha tatu cha Baraza hilo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 tarehe 30 Aprili 2020. Utongani amehamia wilayani humo akitokea Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Baadhi ya Wataalam wakifuatilia kikao cha tatu cha Baraza la Madiwani kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Bahi tarehe 30 Aprili 2020.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa