Serikali imetumia shilingi trilioni 1.09 kutekeleza mpango wa utoaji elimu bila malipo nchini ili watanzania wengi waweze kunufaika na elimu hiyo na kuchangia ukuaji wa uchumi nchini.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo tarehe 04 Agosti wakati akielezea mafanikio ya sekta ya elimu katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma.
“Kazi kubwa tuliyoifanya ni uboreshaji wa miundombinu ya elimu yetu katika maeneo mbalimbali, miundombinu ya shule za msingi na sekondari". Amesema Waziri Jafo.
Rais Dkt. John Magufuli aliona vijana wengi wanahangaika kwa kukosa elimu na alipoingia madarakani alimuhurumia mtoto wa kitanzania na kuamua kutoa elimu bila malipo.
“Tukumbuke kule nyuma kuna vijana waliomaliza kidato cha nne hata vyeti walikuwa wanashindwa kuvipata sababu hawajalipa ada. Hata wengine gharama za mitihani walishindwa kulipia. Watoto wengine walishindwa kumaliza masomo kwa tatizo la ada”. Amesema Waziri Jafo.
Jafo amesema katika kiasi cha fedha zilizotolewa kutekeleza mpango huo, fedha nyingi zimetolewa na Serikali.
“Mara ya kwanza Mheshimiwa Rais alikuwa anatoa shilingi bilioni 20.8 na leo wastani wa shilingi bilioni 23.86 kila mwezi. Ndani ya miaka mitano, Mheshimiwa Rais ameshatoa shilingi trilioni 1.09 kwa ajili ya program ya elimu bila malipo”. Amesema Waziri Jafo.
Waziri huyo amesema kuwa zaidi ya shilingi bilioni 502.2 zimepelekwa katika Elimu ya Msingi na shilingi bilioni 593.9 zimepelekwa kwa ajili ya Elimu ya Sekondari.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa