Afisa uchaguzi wa jimbo la Bahi (RO Jimbo) ndugu. Wiliam Dastan Mpangala amefanya kikao na wadau mbalimbali wa uchaguzi na kuwapa elimu ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura.
katika kikao hichi kilicho jumuisha viongozi mbalimbali wa Wiaya akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Rebecca Nsemwa,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi.Zaina Mlawa,Viongozi wa Dini na madhehebu mbalimbali, Watendaji wa Kata na Vijiji, Wakuu Idara na Vitengo,Machifu na Wazee Maarufu na wakuu wa taasisi mbalimbali. Elimu ya namna ya kuboresha daftari la kudumu la Mpiga Mpiga Kura,vituo vitakavyotumika wakati wa Uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura. Aidha mtoa mada wa kikao hicho ndugu William Mpangala alitoa elimu juu ya utofauti uliopo kati ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura na uandikishaji wa daftari la kupigia kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa jambo ambalo lilikuwa likiwachanganya watu wengi,akitoa ufafanuzi ndugu Mpangala alisema uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura unahusu uandikishaji wa wapiga kura wapya ambao hawakuwahi kuandikishwa kwa kigezo cha umri nk,waliohama maeneo,ambao taarifa zao zilikosewa lakini pia kuondoa wapiga kura walio fariki ambapo mwananchi atapewa kitambulisho kitakachotumika katika uchaguzi mkuu yaani uchaguzi wa madiwani,wabunge na Raisi na zoezi hili hufanyika katika maeneo yaliyoteuliwa na Tume huru ya Uchaguzi WAKATI hivyo uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura haumpi mwananchi uhalali wa kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo mwanachi ili aweze kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa atapaswa kujiandikisha katika kitongoji anachoishi ili kuchagua kiongozi wa kitongoji husika.Elimu hii imeendelea kotolewa kupitia makundi mbalimbali,kwenye mikusanyiko,vijijini,mitandao ya kijamii pamoja na maofisini ili wananchi wawe na uelewa wakutosha juu ya mazoezi haya mawili.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa