Na Benton Nollo, Bahi
Wafugaji nchini wametakiwa kuogesha mifugo yao mara kwa mara ili kupata mazao bora na yenye tija kwao.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akiwahutubia wafugaji na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Uogeshaji Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu lililofanyika katika kijiji cha Bahi Sokoni, wilayani Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020.
Prof. Ole Gabriel amewasisitiza wafugaji kote nchini kuhakikisha kuwa mifugo yao inaogeshwa mara mbili kwa mwezi ili kudhibiti magonjwa yanayoenezwa na kupe ambayo kimsingi yanasababisha hasara kuwa sana kwa wafugaji.
“Ndugu zangu wafugaji uogeshaji wa mifugo wa pamoja ulisimama tangu mwaka 2010 hali iliyosababisha magonjwa yaenezwayo na kupe kuongezeka na kusababisha hasara kwa wafugaji”. Anasema Prof. Ole Gabriel na kuongeza:
“Lakini mwaka 2018 Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilitengeneza mkakati wa kudhibiti magonjwa ya mifugo na ndipo kampeni za uogeshaji mifugo zilianza tena zikiambatana na ukarabati wa majosho, ujenzi wa majosho mapya na kutoa elimu ya kudhibiti magonjwa ya kupe”.
Katibu Mkuu huyo amesema magonjwa hayo yasipodhibitiwa ipasavyo huchangia vifo vya mifugo kwa asilimia 72 ambapo ugonjwa wa Ndigana Kali huchangia vifo vya mifugo kwa asilimia 44 hivyo husababisha hasara ya shilingi bilioni 145, kupunguza uzalishaji wa maziwa, nyama, kushuka kwa thamani ya ngozi, kupoteza wanyama kazi na udumavu wa ndama.
Prof. Ole Gabriel amesema kuwa katika uzinduzi wa Awamu ya Kwanza uliofanyika wilayani Chato mwaka 2018 na Awamu ya Pili uliofanyika Mpimbwe mkoani Katavi Serikali ilinunua lita 21,373 zenye thamani ya shilingi milioni 740.7 na kutosheleza michovyo 254,375,555 ya mifugo yote ikiwemo ngombe 176,320,815, mbuzi 58,012,461, kondoo 20,039,594 na punda 2,685.
“Awamu hii ya Tatu tunazindua Uogeshaji wa Mifugo Kitaifa hapa Bahi, tayari Serikali imeshanunua dawa aina ya Paranex, Paratop na Amitraz lita 15,579 zenye thamani ya shilingi milioni 592.8 za kutosheleza majosho 1,983 katika Halmashauri 162 ambapo tunatarajia michovyo 405,000,000 mpaka zoezi kukamilika”. Amesema Prof. Ole Gabriel.
Tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo Prof. Ole Gabriel ameyataja mafanikio yaliyotokana na zoezi hilo kuwa gharama za uogeshaji kwa wafugaji zimepungua kutoka shilingi 1,000 kwa ng’ombe hadi shilingi 50 kwa ng’ombe na shilingi 10 kwa mbuzi kwa mchovyo mmoja.
Aidha, amesema Serikali Kuu, Halmashauri na wadau imefanikiwa kujenga majosho 101 na kukarabati majosho 578, kuunda kamati 1,036 zinazosimamia shughuli za uogeshaji mifugo ngazi ya josho pamoja na kuunda timu 12 zinazozunguka nchi nzima kuhamasisha shughuli za uogeshaji wa mifugo na ufufuaji wa miundombinu ya mifugo.
Akiwasilisha taarifa ya hali ya mifugo katika Wilaya ya Bahi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Afisa Mifugo na Uvuvi wa Wilaya, Daniel Kehogo amesema kwamba mifugo inachangia zaidi ya asilimia 55 ya mapato ya ndani ya Halmashauri na kwamba ni moja kati ya shughuli kuu mbili za kiuchumi katika wilaya hiyo kwani ina jumla ya ng’ombe 294,235, mbuzi 156,365, kondoo 61,112, punda 9,443, nguruwe 3,504, kuku 327,300, bata 2,912 na kanga 2,623.
Njia hii ya uogeshaji mifugo ili kudhibiti kupe na magonjwa ya kupe ilianza mwaka 1907 wakati wa ukoloni katika josho la Nunge, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma na linaendelea kufanya kazi hadi leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye koti jeupe katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Uogeshaji Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu katika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktroba, 2020.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga (mwenye kilembe) akipokea dawa za ruzuku ya kuogeshea Mifugo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyeshika maiki) kwa niaba ya Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uogeshaji Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu uliofanyika katika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020.
Katibu Mkuu Wizara Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyemshika ng'ombe mkia) akishirikiana na wafugaji katika zoezi la uzinduzi wa kuogesha Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu lililofanyika katika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye koti jeupe) akiweka dawa aina ya Paratop kwenye josho lenye maji, katika zoezi la uzinduzi wa kuogesha Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu lililofanyika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye koti jeupe) akimkagua ndama kupe kabla ya kuogeshwa dawa , katika zoezi la uzinduzi wa kuogesha Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu lililofanyika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020.
Baadhi ya makundi ya mifugo yakisubiri zoezi la uogeshaji katika zoezi la uzinduzi wa kuogesha Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu lililofanyika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020. Ambapo uzinduzi huo ulifanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiwahutubia wafugaji na wananchi waliofika kushuhudia zoezi la uzinduzi wa kuogesha Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu lililofanyika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020.
Baadhi ya wafugaji na wananchi waliojitokeza kushuhudia zoezi la uzinduzi wa kuogesha Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu lililofanyika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020. Ambapo uzinduzi huo ulifanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel.
Katibu Tawala Wilaya ya Bahi akizungumza kabla ya zoezi la uzinduzi wa kuogesha Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu lililofanyika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020. Ambapo uzinduzi huo ulifanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga akiwasalimu wafugaji na wananchi waliojitokeza kushuhudia zoezi la uzinduzi wa kuogesha Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu lililofanyika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020. Ambapo uzinduzi huo ulifanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel.
Afisa Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Bahi, Daniel Kehogo (kushoto aliyevaa kofia) akimkabidhi taarifa ya hali ya mifugo wilayani humo, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel kabla ya zoezi la uzinduzi wa kuogesha Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu lililofanyika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020.
Katibu wa Wafugaji Kata ya Bahi, Yona Paulo akiwasilisha salamu za wafugaji na kuipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuboresha huduma za mifugo nchini katika zoezi la uzinduzi wa kuogesha Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu lililofanyika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020. Ambapo uzinduzi huo ulifanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Bahi Sokoni, akizungumza kabla ya zoezi la uzinduzi wa kuogesha Mifugo Kitaifa Awamu ya Tatu lililofanyika Kijiji cha Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba 2020. Ambapo uzinduzi huo ulifanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel. (Picha zote na Benton Nollo)
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa