Benton Nollo, Ilindi
Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kata ya Ilindi wilayani Bahi wametakiwa kuwa chachu ya Maendeleo katika jamii wanayoishi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda wakati akifunga rasmi mafunzo hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Ilindi tarehe 26 Novemba 2019.
Munkunda amewapongeza wahitimu wote na kuwasihi kuyatumia mafunzo hayo kama chachu ya kujiletea maendeleo na kuhakikisha kuwa wanailinda jamii inayowazunguka. Aidha, amewaahidi kuwa Serikali ipo nao bega kwa bega na ndiyo maana imetumia gharama kubwa kuwapatia mafunzo hayo. Aidha, Munkunda alitumia fursa hiyo kuyaomba makampuni binafsi ya ulinzi kuwatumia vijana hao wenye mafunzo ya kijeshi kwa shughuli zao za ulinzi.
Pia, Munkunda ametumia fursa hiyo kuwaasa vijana wilayani humo kuwa inapotokea fursa kama hiyo katika Kijiji chochote wajitokeze kwa wingi na wasikatishwe tamaa kwani Serikali inatumia gharama kubwa kufanikisha mafunzo hayo.
"Vijana wangu najua mmepitia vikwazo vingi na ninajua mlikatishwa tamaa maana wapo mabingwa wa kukatisha watu tamaa lakini mmevuka salama na leo mnahitimu, basi mafunzo haya yawe na tija katika maisha yenu binafsi na jamii inayowazunguka". Anasema Munkunda.
Mafunzo hayo ya miezi 6 yalijumuisha vijana 92 ambapo kati ya hao wanaume 84 na wanawake 8 chini ya usimamizi wa Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Bahi.
PICHA NA MATUKIO:
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akiwasili katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ilindi kwa ajili ya kufunga rasmi Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kata ya Ilindi tarehe 26 Novemba 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akikagua Gwaride Maalum la Heshima lililoandaliwa kwa ajili yake kabla ya kufunga rasmi Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kata ya Ilindi. Hafla hiyo ilifanyika katika U wanja wa Shule ya Msingi Ilindi tarehe 26 Novemba 2019.
Sajenti Taji Bahati Chizenga akionesha umahiri wa kuzuia pikipiki mbili mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bahi kwenye hafla ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kata ya Ilindi tarehe 26 Novemba 2019.
Afisa Mteule (WO2), Bahati Muro akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Bahi (hayupo pichani) kwenye hafla ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kata ya Ilindi tarehe 26 Novemba 2019.
MG Godliving Urio akisoma risala mbele ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda (hayupo pichani) kwa niaba ya Wahitimu wenzie 92 wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kata ya Ilindi tarehe 26 Novemba 2019.
Gwaride Maalum likipita na kutoa heshima mbele ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kata ya Ilindi tarehe 26 Novemba 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kata ya Ilindi tarehe 26 Novemba 2019.
Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kata ya Ilindi wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi wakati wa hafla za kufunga mafunzo hayo zilizofanyika katika Kijiji cha Ilindi tarehe 26 Novemba 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akikabidhi vyeti vya pongezi katika nyanja mbalimbali kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kata ya Ilindi, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika katika Kijiji cha Ilindi tarehe 26 Novemba 2019.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Bahi wakiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kata ya Ilindi, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika katika Kijiji cha Ilindi tarehe 26 Novemba 2019. (Picha zote na Benton Nollo).
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa