Na. Raymond Gaspary Mhegele
Waza nchini wameaswa kuzingatia lishe bora kwa watoto ili kuwezesha kuondokana na tatizo la utapiamlo. Hayo yamejiri Machi 27, 2025 na Phebronia Ruhaza Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Bahi amesema siku ya lishe ya kijiji wameitumia kutoa mafunzo mbalimbali kwa wazazi na walezi namna ya kuandaa lishe bora kwajili ya watoto pia wazazi wameelekezwa njia bora ya uzazi wa mpango sambamba na Elimu ya ukatili wa kijinsia, matumaini yangu wamama wataenda kufanyia kazi hii kwa kata yetu utapungua kwa namna moja ama nyingine kwa sababu wamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano wamepata elimu ya kutosha kabisa kuhusiana na mambo ya lishe alisema.
Kwa upande wake Ali Abdalaman mkazi wa Bahi mtaa mnadani ameishukuru serikali kwa kuwaletea elimu juu ya lishe jinsi ya kuanda mboga mboga pia tumepatiwa elimu juu ya ukatili wa kijinsia kwa watoto kwani jukumu la kutunza mtoto sio la mama peke yake hata sisi wakina baba ni wajibu wetu.
Naye Tatu Abdala mkazi wa Mbuyuni tunaishukuru serikali yetu utengeneza uji ambao tumefundishwa pia tumekunywa ni uji mtamu tunashukuru tumeambiwa tuwazingatie watoto wetu tunapokuwa majumbani tuwakague pindi tunapowaogesha lakini tusiwaachie malezi wadada wa kazi .
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa