Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo Julai 25, alifanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuona maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri hiyo.
Mhe. Jafo amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Kituo cha afya Bahi na kuweza kukamilika kwa wakati na tayari kimeanza kutoa huduma kwa wananchi.
Akiongelea kuhusu watumishi wa huduma ya afya walioajiriwa hivi karibuni amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tayari imepata watumishi 39 ambao watatawanywa katika Halmashauri hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (Mb) akizungumza na wananchi katika Kituo cha Afya Bahi.
Mhe. Jafo amewaagiza wahudumu wa afya wote nchini kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi ili waweze kuvutiwa kuja kutibiwa kwenye vituo vya afya.
“Nawaagiza Wasimamizi wote wa Vituo vya afya na Zahanati kuhakikisha wanatumia lugha nzuri kwa wagonjwa ili kuwavutia kuja kupata huduma za afya” Alisema Waziri Jafo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akikagua maeneo mbalimbali ya kutolea huduma Kituo cha Afya Bahi.
Amesema kutokana na Halmashauri ya Bahi kuwa na upungufu mkubwa wa vituo vya afya Serikali imeweza kujenga vituo vya afya vya Mundemu na Bahi ili kutoa huduma bora kwa wananchi, pia tayari Serikali imetenga shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya.
Aidha, amewataka wananchi kuhakikisha wanafuata ushauri unaotolewana na wataalam ili kuboresha afya zao.
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ilipokea shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya Bahi, Mundemu na Zahanati ya Chifutuka. Vituo hivyo ni moja kati ya vituo 208 vya kutolea huduma za afya nchini vilivyopatiwa fedha na Serikali kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa