Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengelwa amekabidhi rasmi vyumba vya madarasa 18 Wilayani Bahi katika hafla iliyo hudhuliwa na wadau wa mradi wa shule bora, Watumishi na Wananchi kwa ujumla
Kupitia hafla hiyo Waziri Mchengelwa amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza zaidi katika elimu lakini pia kwa kushirikiana vyema na wadau mbalimbali *toka*(kutoka) mataifa jirani kwa malengo ya kuchochea maendeleo chanya ndani ya jamii na Taifa kwa ujumla
Waziri Mchengelwa amesisitiza Wananchi na serikali kwa ujumla kutumia vyema fursa ya vyumba hivyo vya madarasa kama chachu ya kuzidi kupata matokeo chanya kielimu na kuwataka Wazazi kuwa na muamko chanya dhidi ya Elimu.
Kipekee Mhe. Mchengerwa amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi. Zaina M. Mlawa kwa usimamizi mzuri wa Halmashauri hiyo na kumtaka kuendelea na juhudi hizo, pia amewapongeza maafisa elimu katika Wilaya hiyo hususani Afisa Elimu Msingi Ndugu.Boniface Wilson kwa kushika nafasi ya pili kitaifa katika
matokea ya darasa la saba na Afisa elimu Sekondari Bi. Annette Nara kwa kufanya vizuri matokeo kidato cha pili na cha nne.
Kutokana na ongezeko la madarasa Mkuu wa mkoa Mhe Rosemary Senyamule amekili kusaidia kwa kutoa takwimu zinazo onyesha kupungua kwa kasi ya utoro mashuleni na hii ikichangiwa na Uwekezaji wa Shule bora maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Dodoma.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa