Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amefanya ziara ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kukagua ujenzi wa nyumba yenye uwezo wa kuishi walimu sita kwa mara moja katika Shule ya Sekondari Mpalanga, amezindua Daraja la Chipanga, ametembelea na kukagua ukarabati wa Kituo cha Afya Bahi, ameongea na Watumishi wa Wilaya ya Bahi pamoja na mktano wa hadhara katika Uwanja wa Bahi Sokoni tarehe 19 Oktoba, 2018.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), (wa pili kushoto) akitembea kwa furaha juu ya Daraja la Chipanga lililojengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 2.18 muda mfupi kabla ya kulizindua rasmi tarehe 19 Oktoba, 2018. Wa tatu kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamisi Munkunda na wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bahi, Mhe. Omar Badwel (Mb). (Picha na Benton Nollo).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Daraja la Chipanga lililojengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 2.18 tarehe 19 Oktoba, 2018. Wa tatu kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamisi Munkunda, wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bahi, Mhe. Omar Badwel (Mb) wa pili kulia ni mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Rachel Chuwa na wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya
Chipanga, Mhe. Msafiri Mavunde. (Picha na Benton Nollo).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), (wa tatu kutoka kushoto) akizindua rasmi Daraja la Chipanga lililojengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 2.18 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na shughuli za kijamii wilayani Bahi tarehe 19 Oktoba, 2018. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (Mb), Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamisi Munkunda (mwenye kilemba cheusi), wa pili kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bahi, Mhe. Omar Badwel (Mb). (Picha na Benton Nollo).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika chumba cha upasuaji kilichopo Kituo cha Afya Bahi wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na shughuli za kijamii wilayani Bahi tarehe 19 Oktoba, 2018. Wa kwanza kulia ni Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Dkt. Kassim Kolowa. (Picha na Benton Nollo).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), (wa pili kutoka kulia) akifuatilia na kusikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa kwake na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bahi, Dkt. Kassim Kolowa (wa kwanza kulia) kuhusu taa maalum iliyofungwa kwenye chumba cha upasuaji tayari kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wa kituo hicho wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na shughuli za kijamii wilayani Bahi tarehe 19 Oktoba, 2018. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamisi Munkunda . (Picha na Benton Nollo).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), (wa kwanza kutoka kushoto) akifurahia jambo wakati akizungumza na moja ya akina mama waliofurahishwa na mpango wa Serikali wa kuboresha huduma za afya nchini hasa huduma ya mama na mtoto wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na shughuli za kijamii wilayani Bahi katika Kituo cha Afya Bahi tarehe 19 Oktoba, 2018. (Picha na Benton Nollo).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), (wa kwanza kutoka kushoto) akizungumza na wananchi waliokusanyika katika Kituo cha Afya Bahi wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na shughuli za kijamii wilayani Bahi tarehe 19 Oktoba, 2018. (Picha na Benton Nollo).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Mpalanga mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba ya walimu (yenye uwezo wa kuishi familia sita kwa mara moja) wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na shughuli za kijamii wilayani Bahi tarehe 19 Oktoba, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa