Benton Nollo, Bahi
Wilaya ya Bahi imekuwa wilaya ya pekee kwa Mkoa wa Dodoma kutunukiwa Tuzo ya Utoaji wa Huduma za Afya kwa kuzingatia viashiria vya Mfuko wa Afya wa Pamoja kwa mwaka 2018/2019.
Tuzo hiyo imetolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwenye Mkutano wa 20 wa Kisera wa Sekta ya Afya uliofanyika Jijini Dodoma Novemba 19, 2019 ambapo kati ya Halmashauri 10 za mikoa 7 Tanzania Bara zilizopatiwa tuzo, Wilaya ya Bahi katika Mkoa wa Dodoma ndiyo Wilaya pekee iliyopatiwa tuzo hiyo.
Halmashauri nyingine 9 zilizopata tuzo hiyo zipo katika mikoa ya Mara, Njombe, Arusha, Morogoro, Mbeya na Mtwara.
Tuzo hizo zimetolewa ili kutoa hamasa kwa mikoa na Halmashauri nyingine nchini kutekeleza kwa juhudu na ufanisi viashiria vya Mfuko wa Afya wa Pamoja.
Mkutano huo ulifanyika kwa lengo la kujadili mapendekezo ya vipaumbele vya Kisera kwa mwaka 2020/2021 pamoja na vipaumbele vya Mpango Mkakati wa Tano wa Sekta ya Afya nchini na Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (Mb).
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa