Benton Nollo na Bernard Magawa (DMC), Bahi
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi imewazawadia walimu mahiri fedha, kompyuta na mavazi katika masomo mbalimbali pamoja na shule kumi bora katika mtihani wa Darasa la Saba na Kidato cha Nne ili kutoa motisha kwao kwani kwa matokeo ya Darasa la Saba 2020 Wilaya ya Bahi imekuwa ya kwanza kwa Mkoa wa Dodoma.
Pamoja na zawadi hizo pia, Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa shule kumi duni mwaka 2020 imetoa bendera nyeusi ili ziwakumbushe kwamba wanapaswa kujituma na kuimarisha elimu katika shule zao.
Zawadi hizo zimetolewa kupitia kikao cha wadau wa elimu Wilaya ya Bahi kilichofanyika tarehe 17 Februari 2021 katika uwanja wa Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu.
Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Jeremia Mapogo amewaasa walimu kufanya kazi kwa uadilifu kwani taifa linawategemea sana na kusema kuwa kazi yao niya kipekee kwa kuwa hakuna mtaalamu yeyote ambaye hakupitia mikono ya Mwalimu.
“Mzazi anamzaa mtoto anamlea kwa hatua fulani anamlisha na kuendelea kumpa mahitaji yote, lakini Mwalimu anakuwa na mtoto katika umri wake wote wa kujifunza na anamuandaa tayari kwenda kupambana na maisha yanayotuzunguka hivyo kazi yenu ni nyeti sana.” Amesema Mapogo.
Naye Mbunge wa jimbo la Bahi Kenneth Nollo (Mb) akizungumza katika kikao hicho amesema hatamfumbia macho mtu yeyote atakayeshiriki kumpa ujauzito msichana wa shule na kuahidi kupambana kwa uwezo wake wote kutokomeza tatizo hilo.
Akizungumza na walimu katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga amewaonya walimu kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi badala yake wazingatie maadili ya kazi yao ili wawe na ufanisi katika kazi zitakazoiwezesha halmashauri kuendelea kulinda kiwango cha elimu walichokifikia kwa sasa.
Awali, akitoa taarifa kuhusiana na tuzo hizo, Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Bahi, Boniface William amesema zawadi zilizotolewa zimehusisha Walimu mahiri katika masomo mbalimbali kwa shule za Msingi na Sekondari yakiwemo masomo ya Hisabati, Sayansi, Fizikia, Siasa, Kemia na masomo mengine pamoja na kuzawadia shule kumi bora na kumi duni kwa shule za msingi na sekondari katika matokeo kwa mwaka wa masomo 2020.
Picha na Matukio:
Picha zote juu ni zawadi kwa shule na walimu wa masomo waliofanya vizuri kwenye mitihani ya taifa ya mwaka 2020 shule za msingi na sekondari wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilaya ya Bahi kilichofanyika tarehe 17 Februari 2021..
Picha zote za juu ni walimu wa shule zilizofanya vibaya kwenye mitihani ya taifa ya mwaka 2020 shule za msingi na sekondari wakipokea bendera nyeusi wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilaya ya Bahi kilichofanyika tarehe 17 Februari 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilaya ya Bahi kilichofanyika tarehe 17 Februari, 2021.
Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Bahi, Boniphace William akiwasilisha taarifa ya elimu msingi na sekondari kwa mwaka 2020 wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilaya ya Bahi kilichofanyika tarehe 17 Februari 2021.
Mthibiti Ubora wa Shule Wilaya ya Bahi, Pudenciana Kuzenza akiwasilisha tathmini ya ubora wa shule za msingi wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilaya ya Bahi kilichofanyika tarehe 17 Februari 2021.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Donald Mejiti akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilaya ya Bahi kilichofanyika tarehe 17 Februari 2021.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Pius Mwaluko akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilaya ya Bahi kilichofanyika tarehe 17 Februari 2021.
Mbunge wa Jimbo la Bahi, Kenneth Nollo (Mb) akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilaya ya Bahi kilichofanyika tarehe 17 Februari 2021.
Picha zote za juu ni viongozi na wadau wa elimu wakitoa mawazo yao juu ya namna ya kuboresha sekta ya elimu ili kukuza ufauli wilayani Bahi wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilaya ya Bahi kilichofanyika tarehe 17 Februari 2021.
Baadhi ya Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu wakitoa uzoefu kwa namna walivyofanikisha kuongeza ufaulu katika mitihani ya taifa ya mwaka 2020 wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilaya ya Bahi kilichofanyika tarehe 17 Februari 2021.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa