Na Benton Nollo, Bahi
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Bahi, Dkt. Fatuma Mganga amewaagiza BVR Kit Operators na Waandishi Wasaidizi kujiepusha na ulevi ili zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili lisiwe na dosari yoyote.
Dkt. Mganga ameyasema hayo tarehe 30 Aprili 2020 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Bahi, wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa BVR Kit Operators na Waandishi Wasaidizi 45 waliochaguliwa kwa ajili ya zoezi hilo litakalofanyika katika Kata 22 za wilaya hiyo kuanzia tarehe 02 hadi tarehe 04 Mei, 2020.
“Twende kule tukajiheshimu tuwe na maadili ya hali ya juu, hata kama wewe ni mlevi yaani kwa siku hizi ngapi hakikisha kwamba hujihusishi na ulevi ili uweze kufanya kazi ya watu vizuri”. Anasema Munkunda.
Aidha, pamoja na tahadhali hiyo Dkt. Mganga amewakumbusha BVR Kit Operators na Waandishi Wasaidizi kuchukua tahadhali dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na Virusi vya Corona katika kipindi chote cha uboreshaji wa Daftari hilo.
Dkt. Mganga amesema kuwa kutokana na ugonjwa huo zipo nchi duniani zimezuia watu wake kutoka nje na kwa kufanya hivyo nchi hizo zimeathirika sana kiuchumi kwani shughuli za uzalishaji mali zimesimama.
“Lakini kwa maono mapana ya Rais wetu, ameona ni vema sisi tukaendelea na michakato ya shughuli zetu kwa kuchukua tahadhali, maanaake tunafahamu ugonjwa unaambukizwaje, tukichukua tahadhali na huku tunaendelea kufanya kazi, hatutayumbisha uchumi wa nchi yetu”. Anasema Dkt. Mganga na kuongeza;
“Michakato mingi ambayo inatakiwa kufanyika itaendelea kama kawaida na hasa tukizingatia mwaka huu ndiyo mwaka wa uchaguzi…ni lazima tuchukue tahadhali za kujikinga sisi wenyewe na wateja wetu watakaokuja kuboresha taarifa zao.
Dkt. Mganga amewasisitiza BVR Kit Operators na Waandishi Wasaidizi kujikinga na ugonjwa huo kwa kuvaa Barakoa wakati wote wawapo vituoni mwao na kuwaelekeza wananchi wanaokwenda kuboresha taarifa zao kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni na kupaka vitakasa mikono ambapo vifaa vyote hivyo alisema vimetolewa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika vituo vyote 22 ili kuwakinga na kuwalinda wananchi dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona katika kipindi chote cha zoezi hilo.
“Watu wasisonamane kituoni, toeni maelekezo ya watu kukaa mbalimbali na hakikisha kila wakati kwenye kituo chako kuna maji na sabuni…maji yakiisha zoezi lisiendelee mpaka maji yamepatikana na hata wakati wa kuelekezana msikalibiane na muwaelimishe wananchi kwa upendo ili watambue na kuelewa umuhimu wa kunawa mikono na isionekane kuwa kwa wao kunawa mikono wananyanyapaliwa”. Anasema Dkt. Mganga.
Baadhi ya Washiriki katika Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili (BVR Kit Operators na Waandishi Wasaidizi) wakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Afisa Mwandikishaji Jimbo la Bahi, Dkt. Fatuma Mganga (hayupo pichani) kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe 30 Aprili 2020.
Baadhi ya Washiriki katika Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili (BVR Kit Operators na Waandishi Wasaidizi) wakiapa kiapo cha utii kwenye mara baada ya Hotuba ya Ufunguzi katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe 30 Aprili 2020.
Wasimamizi Wasaidizi Ngazi ya Wilaya wakitoa maelekezo na ufafanuzi kwa Washiriki wa Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili (BVR Kit Operators na Waandishi Wasaidizi) kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tarehe 30 Aprili 2020. Zoezi hilo la siku tatu linafanyika kuanzia terehe 02 hadi tarehe 04 Mei 2020 katika Kata zote 22 za wilaya hiyo.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa