• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
BAHI DISTRICT COUNCIL
BAHI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kazi na Moto
      • Afya
      • Maji
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia na Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mpiango
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokubaliwa
    • Miradi Inayoendelea
      • TASAF
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Kazi
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbali Mbali
    • Miongozo Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video Mbali Mbali
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

INEC kushirikiana kwa karibu na vyombo vya habari katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025

Imechapishwa: August 4th, 2025

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeahidi kutoa ushirikiano wa karibu kwa vyombo vya habari nchini katika kuhakikisha taarifa za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 zinapatikana kwa wakati na kwa usahihi.

Akifungua mafunzo ya Wahariri na Waandishi wa Habari kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 katika ukumbi wa Mlimani City leo tarehe 4 Agosti 2025, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndugu Kailima R.K., amesema katika kipindi hiki cha uchaguzi, Tume itashirikiana na waandishi wa habari kupitia njia mbalimbali ikiwemo kushiriki katika vipindi vya redio na televisheni, pamoja na kutoa taarifa rasmi kwa wakati unaofaa ili kuwahakikishia wananchi upatikanaji wa habari za kweli na zisizo na upotoshaji.

“Tunaamini kuwa vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa amani. Kwa hiyo, tutaendelea kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha habari zinazotolewa zinazingatia maadili ya uandishi wa habari na kuepuka maudhui yanayoweza kuchochea chuki au ghasia,” amesema Ndugu Kailima. Mkurugenzi wa Uchaguzi amesisitiza kuwa Tume itatoa taarifa sahihi na kwa wakati, na itatoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kila wanapohitaji ufafanuzi au msaada wowote wa kihabari.

Aidha, Ndugu Kailima ameeleza kuwa Tume itazindua mfumo wa kusajili vyombo vya habari kuanzia tarehe 1 hadi 30 Septemba 2025.

“Mfumo huu utasaidia vyombo vya habari kupata vibali na vitambulisho rasmi vya waandishi wake kwa ajili ya kufanikisha kazi zao wakati wa Uchaguzi Mkuu,” ameeleza.

Kufanyika kwa mafunzo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari kumehitimisha mfululizo wa mikutano ya wadau ambayo ilianza tangu tarehe 27 Julai 2025, ambapo Tume ilikutana na viongozi wa vyama vya siasa, asasi zisizo za kiserikali, wawakilishi wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, wahariri wa vyombo vya habari, waandishi wa habari na watayarishaji wa maudhui ya mtandaoni.


Taarifa hiii imetolewa na INEC kupitia tovuti (https://www.inec.go.tz/)

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI. July 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO May 07, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI May 02, 2025
  • Mikopo ya Hazina Kwa Watumishi wa Umma October 27, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Waandishi wa habari wahimizwa kuhamasisha ushiriki wa wananchi kupiga kura

    August 02, 2025
  • INEC kushirikiana kwa karibu na vyombo vya habari katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025

    August 04, 2025
  • WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA (AROs) WAPATA MAFUNZO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2025

    August 04, 2025
  • MHE.NYINGO AKUTANA NA TIMU YA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA (CHMT) PAMOJA NA WAGANGA WAFAWIDHI WA HOSPITAL,VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI.

    July 29, 2025
  • Tazama Zote

Video

Jinsi ya kuomba uhamisho kwenye mfumo wa Utumishi
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tazama na Kudownload Orodha ya Walioitwa Kwenye Interview kwa Nafasi za Watendaji wa Vijiji Bahi
  • Matokeo Kidato cha Nne 2017
  • Tazama matokeo ya Darasa la saba 2019 ya shule zote za Bahi
  • Tazama na Kudownload vigezo vya Nafasi za Kazi kwa Watendaji wa Vijiji
  • Matokeo ya QT
  • 1: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • Vendor Form
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • NECTA
  • Mfumo wa uhamisho kwa watumishi,Mikopo na Kupata Salary Slips
  • Utumishi
  • OR-TAMISEMI
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Dodoma

Watembeleaji wa Nje

world map hits counter

Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitengo cha Ugavi na Manunuzi

    Anuani: S.L.P 2993 DODOMA

    Simu: +255 762077589

    Simu: +255 762077589

    Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa