Na Benton Nollo, Bahi
Walimu nchini zimetakiwa kutowazuia wanafunzi kuandikishwa Darasa la Kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2020 kwa sababu ya kukosa Cheti cha Kuzaliwa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (Mb), wakati wa ziara yake Wilayani Bahi kukagua uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la Kwanza kwa shule za msingi pamoja na mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika shule za sekondari tarehe 07 Januari 2020.
Jafo amesema ni marufuku mwanafunzi kuzuiliwa kuandikishwa Darasa la Kwanza kwa sababu ya kukosa Cheti cha Kuzaliwa.
Amesema amepokea malalamiko kutoka katika baadhi ya maeneo nchini kuwa wanafunzi wa Darasa la Kwanza hawaandikishwi kama hawana vyeti vya kuzaliwa.
“Nimeona nitoe ufafanuzi kuhusu suala hili kuwa cheti cha kuzaliwa ni haki ya kila mtoto lakini isimzuie mtoto huyo kuanza shule eti kwa sababu tu hajapata cheti hicho; Watoto wote wapokelewe, waandikishwe na waanze masomo huku wazazi wao wakiendelea na mchakato wa kuwatafutia vyeti hivyo”. Amesema Jafo na kuongeza.
“Sitaki kusikia eneo lolote nchini mtoto ameachwa kupokelewa kuanza shule kwa sababu ya kukosa cheti cha kuzaliwa, mzazi ahakikishe ndani ya miezi minne amepata cheti hicho lakini mtoto huyo aanze masomo mara moja wakati masuala ya cheti yanaendea kushughulikiwa na mzazi kwenye mamlaka husika”.
Akizungumza wakati akikagua mapokezi ya Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari Bahi Wilayani humo amesema wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika muda uliopangwa na wapokelewe bila masharti ya kuleta dawati, unga, mahindi au maharage.
Ambapo aliongeza kuwa Walimu watambue Serikali inatoa Elimumsingi bila malipo hivyo, kila mwanafunzi anatakiwa kupata elimu bila bughudha yoyote.
Waziri Jafo amepongeza uongozi wa Wilaya ya Bahi kwa umakini waliouonyesha katika zoezi zima za uandikishaji wa Darasa la Kwanza linaloendelea na maandalizi mazuri ya kuwapokea wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, na hata katika usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya hiyo hasa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Bahi mjini na Vituo vya Afya vitatu vya Bahi, Mundemu na Chifutuka.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda amesema katika Halmashauri ya Bahi walishafanya kampeni ya upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano hivyo, watoto wengi wanaoanza shule hivi sasa wanavyo vyeti hivyo na endapo ikitokea kuna mtoto hana cheti basi ataandikishwa shule ndipo mchakato wa kupata cheti hicho utafuata.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Charles Mduma amemueleza Waziri Jafo kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza katika Wilaya ya Bahi ni 2,712.
Mduma alisema kuwa changamoto iliyokuwepo ni uhaba wa madawati ambayo tayari Halmashauri imeshaanza kuchonga madawati yatakayokidhi idadi ya wanafunzi hao.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkakatika, John Laurent Josephat amesema shule yake ina lengo ya kaundikisha wanafunzi 180 na kwa siku ya kwanza tu baada ya shule kufunguliwa tarehe 06 Januari 2020, shule hiyo imeandikisha wanafunzi 134 sawa na asilimia 70.
“Wanafuzi wote walioletwa shuleni kwetu tumewaandikisha na endapo mtoto hana cheti cha kuzaliwa tulitumia Kadi ya Kliniki kupata taarifa sahihi za mtoto na hatujarudisha mwanafunzi hata mmoja wote wamepokelewa na wameanza masomo”. Alisema Mwl. Josephat.
Shule ya Msingi Mkakatika, katika matokeo ya Darasa la Saba kwa mwaka 2019 ilishika nafasi ya kwanza kiwilaya na kimkoa ilishika nafasi ya tatu.
Picha na Matukio:
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (Mb), akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya ziara ya siku moja kukagua uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la Kwanza kwa shule za msingi pamoja na mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika shule za sekondari tarehe 07 Januari 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda (kushoto) akitoa taarifa ya uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la Kwanza kwa shule za msingi pamoja na mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika shule za sekondari kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (Mb) (kulia) tarehe 07 Januari 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (Mb), akiwa katika Shule ya Sekondari Bahi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja kukagua uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la Kwanza kwa shule za msingi pamoja na mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza shule za sekondari, tarehe 07 Januari 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (Mb), (wa tatu kushoto), akipokelewa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkakatika, John Laurent Josephat (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili shuleni hapo akiwa katika ziara ya kukagua uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la Kwanza kwa shule za msingi pamoja na mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza shule za sekondari, tarehe 07 Januari 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (Mb), akiwa Shule ya Msingi Mkakatika wilayani Bahi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja kukagua uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la Kwanza kwa shule za msingi pamoja na mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza shule za sekondari, tarehe 07 Januari 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (Mb), akiwa na wanafunzi wa Darasa la Kwanza wa Shule ya Msingi Mkakatika, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja kukagua uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la Kwanza kwa shule za msingi pamoja na mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza shule za sekondari, tarehe 07 Januari 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (Mb), akiwa katika moja ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Bahi ambapo baada ya ziara yake ya kukagua uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la Kwanza kwa shule za msingi pamoja na mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza shule za sekondari, tarehe 07 Januari 2020, pia alipita kukagua mandhari ya hospitali hiyo baada ya kukamilika.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa