Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amekemea mikusanyiko ya watoto (Madrasa na Sunday Schools) inayofanyika kwenye nyumba za ibada wakati akizungumza na viongozi wa mikoa kwa njia televisheni ifisini kwake Dodoma tarehe 15 Aprili 2020. Amesema kuwa imebainika kwamba baada ya masomo kusitishwa kwa sababu ya ugonjwa wa Covid 19 watoto wamekuwa wakienda kanisani na misikitini kwa ajili ya kujifunza.
"Naambiwa pamoja na kibali cha taasisi za dini kuendelea kumeanza mfumo wa kuanzisha madarasa ya watoto wadogo kwenye misikiti na makanisa inaitwa Sunday School inawakusanya vijana wengi, watoto wengi hilo pia ni sehemu ya maeneo ambayo tumeyawekea Kalantini hatutakuwa na Sunday School huo ni msongamano. Anasema Waziri Mkuu Majaliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa amesisitiza kuwa alipokutana na Maaskofu na Mashekh walikubaliana kusitisha huduma nyingine zote isipokuwa Ibada tu.
"Tumeruhusu Ibada tu... na ibada hiyo lazima iangaliwe iwe fupi inavyowezekana, tumezungumza vizuri na Mababa Askofu, tumezungumza pia vizuri na Mamufti wetu wa Tanzania Bara pamoja na wa Zanzibar kuhakikisha kwamba madrasa madrasa zinazoendeshwa humo, hizo Sunday Schools zote huwa hazipo, tulichoacha ni ibada". Anasema Waziri Mkuu Majaliwa.
Amesema ni marufuku kwa watoto kukusanywa kwa kisingizio cha Sunday Schools au Madrasa. Amesema katika mazungumzo hayo kilichoachwa ni ibada ili ibada hizo zisaidie waumini kuliombea Taifa na amesema Serikali imesisitiza katika nyumba hizo za ibada waumini wake wajali kukaa kwa nafasi kama Wataalam wa Afya wanavyoshauri na tena ibada iwe kwa muda mfupi na baada ya ibada waumini watawanyike mara moja.
Pia, Waziri Mkuu Majaliwa amesema makanisa ua misikiti haiwezi kuendesha makongamano ya kidini hivi sasa kwa sababu kongamano linahusisha watu wengi na wanatoka katika maeneo mbalimbali ambapo hiyo ni njia rahisi sana kupeleka maambukizi ya Covid 19.
"Tusingependa sana tuingilie masuala ya dini lakini tunaamini Mababa Askofu, Mheshimiwa Mufti wa Bara na Zanzibar wanaelewa vizuri jambo hili na wao wataendela kutusaidia kuliratibu vizuri ili lisiweze kuleta madhara makubwa". Anasema Waziri Mkuu Majaliwa.
Pamoja na katazo hilo, Waziri Mkuu Majaliwa aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali inatambua kuwa kuna masoko, maduka, Super Market na haikusudii kusitisha huduma hizo za kupata bidhaa kwenye maduka lakini muhimu zaidi, maduka yote yaweke ndoo za maji kwenye mlango na mteja anapoingia ndani awe ameshanawa ili anapochagua bidhaa ndani ya duka mikono yake iwe misafi na ikiwezeka hata anapotoka anawe.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa