Chuo cha VETA Bahi kina ukubwa wa eneo la hekari 52 na mpaka sasa kimeshakamilika katika hatua ya ujenzi na kupangiwa kutoa mafunzo kwenye kozi sita za ufundi stadi kama ifuatavyo:-Ufundi wa ujenzi (Masonry and bricklaying).
,Uchomeleaji wa vyuma (Welding and metal fabrication),Ushonaji (Toiloring),Uhazili na kompyuta (Secrtarial and computer application),Ufundi umeme wa mjumbani (Electrical Installation),Ufundi wa magari (Motor vehicle mechanics).
chini ya uongozi wa serikali ya awamu sita Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani alitoa kiasi cha shilingi Bilioni 2.7 kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho ili kusogeza huduma ya elimu ya fundi kwa wananchi wa wilaya ya bahi. Mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe. Godwin Gondwe aliwataka wananchi,wananfunzi na viongozi kumuunga mkono Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa juhudi za Maendeleo anazoendelea kuchukua .
Akishirikiana na viongozi mbalimbali wa Halmashauri wakiwemo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Donald Mejiti,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi.Zaina Mlawa pamoja na wakuu wa idara na vitengo aliongoza zoezi la upandaji miti miche 200 katika chuo hili ili kudumisha utunzaji wa mazingira ya chuo hicho,pia mkuu wa wilaya hiyo Mhe.Godwin Gondwe amewataka wanachi wa wilaya hiyo kuktumia chuo hicho kama fursa ya watoto wao kupata ujuzi na maarifa ili waweze kujiajiri nakujipatia kipato.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa