Na Benton Nollo, Nondwa
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda ameipongeza Menejimenti na Halmashauri ya wilaya hiyo kwa kujenga madarasa manne (4) na ofisi mbili (2) za walimu katika Shule ya Sekondari mpya ya Nondwa kwa shilingi milioni 72 ambazo ni mapato ya ndani.
Munkunda ameyasema hayo alipotembelea ujenzi huo tarehe 05 Mei 2020 akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo.
Pamoja na kuipongeza Halmashauri kwa kutoa fedha za mapato ya ndani shilingi milioni 55 kumalizia ujenzi wa majengo hayo, pia Munkunda aliwapongeza wananchi wa Vijiji vya Nondwa na Zejele kwa mchango wa shilingi milioni 17 ambazo ni jitihada zao katika kuanzisha ujenzi huo.
“Viongozi wenzangu kama tunavyofahamu Kata ya Nondwa haina shule ya Sekondari hivyo, inawalazimu wanafunzi wa Nondwa na Zejele kutembea umbali wa takriban kilomita 20 kila siku kufuata masomo katika Shule ya Sekondari Chikopelo iliyopo Kata jirani ya Chali”. Anasema Munkunda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi kwa mchango wa mifuko 15 ya saruji aliyoitoa wakati wa ziara hiyo na kuisisitiza Kamati ya Ujenzi kuendelea na michango zaidi ili kukamilisha ujenzi wa choo ili shule ianze.
“Wenyeviti wa Vijiji wa Zejele na Nondwa wote mpo…jamani shime tumeshaona dalili kwamba shule yetu inaanza, tujenge vyoo lakini madarasa manne hayatoshi tujue kwamba hapa ndo tumeanza mchaka mchaka, shule kufikia Kidato cha Kwanza hadi cha Nne ni madarasa yasiyopungua hata kumi tufahamu hilo…na hivi sasa watoto wanafaulu kwa sababu elimu imeboreshwa sana”. Anasema Dkt. Mganga.
Aidha, Wenyeviti wa Vijiji, Bernald Majuto (Nondwa) na Samsoni Mkwawi (Zejele) wameishukuru sana serikali kupitia Halmashauri hiyo kwa kuleta fedha hiyo ambayo imefanikisha ujenzi wa madarasa hayo pamoja na ofisi za walimu na wamewahakikishia viongozi hao kuwa ndani ya siku 30 vyoo vitakuwa vimekamilika.
Pia, viongozi hao wameahidi kwamba kwa kuwa jambo hilo limewafurahisha sana wananchi na wapo tayari kuchangia, hivyo kuanzia mwezi Juni 2020 Serikali za Vijiji zote mbili zimeshaweka mikakati ya kuanza michango ili kuanza ujenzi wa madarasa mengine mawili na ofisi ya walimu.
Muuonekano wa madarasa manne (4) na ofisi mbili (2) za walimu ambapo majengo hayo yapo katika hatua za umaliziaji.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akizungumza na viongozi wa Kata ya Nondwa (hawapo pichani) mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne (4) na ofisi mbili (2) za walimu kwa ajili ya shule mpya ya Sekondari Nondwa ambapo majengo hayo yapo katika hatua za umaliziaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga akizungumza na viongozi wa Kata ya Nondwa (hawapo pichani) mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne (4) na ofisi mbili (2) za walimu kwa ajili ya shule mpya ya Sekondari Nondwa ambapo majengo hayo yapo katika hatua za umaliziaji.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wakikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne (4) na ofisi mbili (2) za walimu katika shule mpya ya Sekondari Nondwa ambapo majengo hayo yapo katika hatua za umaliziaji.
Afisa Tarafa Chipanga, Christian Kiiza (kushoto) akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Bahi kwa kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne (4) na ofisi mbili (2) za walimu kwa ajili ya shule mpya ya Sekondari Nondwa ambapo majengo hayo yapo katika hatua za umaliziaji.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nondwa, Bernald Majuto (kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda (hayupo pichani) aliyoifanya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne (4) na ofisi mbili (2) za walimu kwa ajili ya shule mpya ya Sekondari Nondwa ambapo majengo hayo yapo katika hatua za umaliziaji.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Zejele, Samsoni Mkwawi akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda (hayupo pichani) aliyekuwa akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne (4) na ofisi mbili (2) za walimu kwa ajili ya shule mpya ya Sekondari Nondwa ambapo majengo hayo yapo katika hatua za umaliziaji.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa