Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi amezindua mafunzo ambayo yatadumu kwa siku sita kuanzia tarehe 26 march 2025 mpaka tarehe 31 march 2025.
Ni Mafunzo ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi wanayo pewa walimu wakuu wa shule za msingi,Maafisa elimu Kata, walimu wa Mazingira,Maafisa Maendeleo,Maafisa Tarafa na wadhibiti ubora, Mafunzo yamehusisha ujifunzaji wa mada mbalimbali kuhusu mazingira lakini pia mafunzo kwa vitendo ikiwemo kutembelea baadhi ya mazingira ya mfano.
Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo washiriki wote juu ya namna nzuri zaidi ya Upandaji miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi lakini pia sambamba na elimu toka Shule bora dhidi ya ujenzi bora wa Madarasa ili kupunguza kiwango cha joto na kuleta mzunguko mzurii wa hali ya hewa.
Utoaji Elimu kwenye mafunzo haya umehusisha watoa mada mbalimbali ikiwemo wakiwemo TFS,Uongozi toka Shule bora (Mkuu wa shule bora Dodoma ndugu Mtemi zombwe), Mhadhiri toka Tengeru (Agnes Kapinga), Maafisa Mazingira pamoja na wahandisi toka Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa