Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi amefanya ziara na kutembelea shule ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia maarufu kama kigwe viziwi na kuwapelekea mahitaji ya chakula ambapo alikabidhi mbuzi wawili na kisha kupata picha ya pamoja na wanafunzi hao pamoja na walimu. Ziara hiyo iliambatana na ufuatiliaji wa ujenzi wa uzio katika shule hiyo ambayo ilipokea fedha kutoka serikalini kwa ajikibyabujenzi wa uzio huo ili wanafunzi wapate mazingira salama ya kujifunzia. Aidha, Mkurugenzi mtendaji alitembelea wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita nakuwapa vifaa vya michezo ikiwa kudumishabna kuboreha afya zao kupitia michezo, pia aliwapa nasaha kuto sahau kutimiza wajibu wao kama wanafunzi na kuwasihi wafanye bidii katika masomo yao
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 687748878
Simu: +255 687748878
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa