Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha miundo mbinu ya elimu kote nchini kwa kutoa fedha za ukarabati wa miundo mbinu chakavu lakini pia ujenzi wa miundo mbinu mipya katika Halmashauri mbalimbali hapa nchini Tanzania ikiwemo madarasa mapya pamoja na vyoo.
Halmshauri ya Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa almashauri zinazonufaika na uboreshaji huo ambapo mwaka huu 2024 imepokea kiasi cha shilingi 2,516,200,000/= ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 95 Pamoja na matundu ya vyoo 84 katika shule za sekondari 23 wilayani Bahi. Hii imesemwa katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya bahi kilichoitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Godwin Gondwe akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri hiyo Bi.Zaina Mlawa na viongozi wa ngazi mbalimbali wialayani humo kwa ajili ya kuwapa taarifa wakuu wa shule za sekondari juu ya mapokezi ya fedha hizo ambazo lengo kuu ni kuimarisha miundombinu ya madarasa katika sekta ya elimu ndani ya wilaya hiyo.
Mhe.Godwin Gondwe amewapa maelekezo wakuu wa shule hao kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kusimamia mradi huo kutekelezwa katika ubora wa hali ya juu na kwa wakati katika kikao hicho Mhe.Godwin Gondwe kwa niamba ya uongozi mzima wa wilaya hiyo amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimbuka wilaya ya bahi na watu wake kwa kuendelea kuwaletea fedha za maendeleo kila mwaka wa fedha. Aidha amewasihi wanachi kumuunga mkono katika juhudi zake za kuiletea maendeleo wilaya hiyo ikiwa kuitunza miundo mbinu hiyo na kuhakikisha wanafunzi wanapelekwa shuleni kwa wakati.
WAJUMBE WALIOSHIRIKI KIKAO HICHO NI; -
1. Wakuu wa shule
2. Waratibu elimu Kata
3. Wenyeviti wa Vijiji
4. Maafisa Elimu
5. Wakuu wa idara husika - Ujenzi,PMU,Elimu Sekondari na Maendeleo ya Jamii
7. Kamati ya ulinzi na usalama (W)
Wajumbe hao walioshiriki walipitishwa na Mhe.Godwin Gondwe Mkuu wa Wilaya ya Bahi katika mpangokazi wa ujenzi kuanzia Kazi za awali Hadi hatua ya umaliziaji wa mradi huo
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa