Umoja wa shule za msing Tanzania TAPSHA (Tanzania Primary School Head Teachers) wamefanya mkutano mkuu ikiwa ni pamoja na kujipongeza kwa kwa kufanya vizuri katika matokea ya darasa la saba kwa mwaka 2023/2024.
Mgeni rasmi Dkt. Charles E. Msonde amempongeza Mkuu Wilaya hiyo Mhe.Godwini Gondwe kwa kuonesha ushirikiano mkubwa kwa uongozi wa Halmashauri na kumtaka kuendelea na ushirikiano huo kwani ndio chachu ya mafanikio,pia Dkt.Charles Msonde wasifu walimu wakuu hao kwa kufanya kazi kwa bidi ambapo kupitia mkutano huo aliwapa walimu wakuu hao salamu za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Pia,Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Godwin Gondwe pamoja uongozi wa Halmashauri ya Bahi walimpongeza kipekee kabisa Afisa Elimu Msingi Ndg. Boniface Wilson
Kwa juhudi zake na ushirikiano alionao kwa walimu katika wilaya hiyo. Mhe. Gondwe alienda mbali Zaidi na kumuomba Mgeni rasmi Dkt.Charles Msonde ikimpendeza aone namna ya kumuinua Afisa elimu huyo na kumpa ngazi ya juu Zaidi kwani kazi yako iko wazi na anaifanya kwa weledi mkubwa na kuletwa mchango usio nashaka.
Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa elimu pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya walimu wakuu wameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidi ambapo waliongozwa na kauli mbiu iliyosema “Kujitoa na kuthubutu ni chachu ya mafanikio”.
Kwa taarifa zaidi na picha za matukio tembelea tovuti www.bahidc.go.tz
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa