Watanzania takriban milioni 29 wanatarajia kupiga kura Jumatano tarehe 28 Oktoba, 2020 katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania.
Jumla ya Wapiga kura 29,188,348 wameandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Taifa ya Uchaguzi - NEC na Wapiga kura 566,352 wameandikishwa katika Daftari la Wapiga kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Da es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema katika uchaguzi huo kuna vituo vya kupigia kura 81,567 vikiwemo vituo 80,155 vinavyokana na Daftari la Kudumu la Wapiga kura NEC na vituo 1,412 vinavyotokana na Daftari la Wapiga kura la ZEC.
Vilevile, amesema kuwa vyama vyote 19 vyenye usajili wa kudumu vitashiriki ambapo kwa mujibu wa takwimu kuna jumla ya wagombea 1,257 katika nafasi za ubunge na jumla ya wagombea 9,237 katika nafasi za udiwani.
Jaji Kaijage amesema kuwa vituo vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa