Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekoma rasmi leo kuendelea na shughuli za kikazi mara baada ya Rais Mteule, Dkt. John Magufuli kuapishwa kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma jana, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya kuapishwa kwa Rais Mteule, Dkt. Magufuli.
Dkt. Abbas amesema kuwa kisheria ni kwamba Baraza la Mawaziri la kipindi cha 2015 - 2020 mwisho wake ni mara tu Rais Mteule atakapoapishwa kushika kipindi chake cha pili cha miaka mitano. Baada ya hapo majukumu yote yatafanywa na Makatibu Wakuu wa Wizara hadi atakapotangaza baraza jipya la Mawaziri.
Chanzo: CCM Blog
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa