Serikali imewahakikishia Watanzania kuwa hakuna upungufu wa sukari nchini hivyo, wananchi wasiwe na wasiwasi.
Kauli hiyo ametolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (Mb), wakati akitoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu kupanda kwa bei ya sukari tarehe 16 Aprili jijini Dodoma.
Bashungwa amesema kuwa kila mwaka serikali imekuwa makini katika kutathmini mahitaji ya sukari kwa wananchi na uwezo wa viwanda vya ndani katika uzalishaji wa bidhaa hiyo muhimu kwa jamii.
Hata hivyo, Bashungwa amesema ni kweli bei ya sukari imepanda lakini haisababishwi na upungufu wa sukari bali imesababishwa na waagizaji kushindwa kuagiza kwa wakati kutokana na ugonjwa wa Homa ya Mapafu Covid 19 unayosababishwa na virusi vya Corona.
“Ili kukabiliana na kadhia hiyo Serikali imetoa vibali vya jumla ya tani 40,000 kwa kampuni 4 za wazalishaji ambapo kila kampuni imeagiza tani 10,000”. Amesema Waziri Bashunga.
Aidha, Bashungwa amesema kuwa tayari sukari iliyokwisha ingia bandarini kupitia kampuni ya Kagera Sugar ni tani 9,990 na imeanza kutolewa bandarini tangu tarehe 15 Aprili 2020.
Pia, Bashungwa amesema tarehe 24, 28 na 30 mwezi Aprili 2020 Kampuni ya Mtibwa Sugar itaingiza Tani 10,000 na Kampuni ya Kilombero Sugar itaingiza tani 1,624 hivi karibuni kutoka Malawi na Msumbiji huku tani 1,800 ikiagizwa kutoka Afrika Kusini.
“Wiki ya kwanza ya mwezi Mei, 2020 Kampuni ya Kilombero Sugar itaingiza tani 7,276 huku tarehe 15 Mei 2020 Kampuni ya TPC itaingiza tani 5,000 na tarehe 30 Mei 2020 tani 4,500 zitaingia nchini”. Amebainisha Waziri Bashunga.
Katika hatua nyingine, Bashungwa amesema kuwa Wizara inatarajia kuomba nyongeza ya Tani 58,000 ili kukidhi mahitaji ya sukari kufikia Juni 2020.
Hata hivyo, amesema kuwa asilimia 80 ya sukari ambapo kwa mujibu wa takwimu mahitaji ya sukari inayotumiwa nyumbani ni tani 4,700,000 ambapo kati ya hizo tani 378,000 zinazalishwa nchini na ameeleza kwamba hiyo ni hatua kubwa kwa nchi na serikali katika mkakati wa kuimarisha uchumi wa viwanda huku wawekezaji wengi wakiendelea na mchakato wa uongezaji tija na uwezo wa uzalishaji.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa