Katika kipindi cha miaka mitano, Serikali ya Awamu ya Tano imetumia takribani shilingi trilioni 3.463 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya barabara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo wakati wa kuelezea mafanikio katika sekta ya miundombinu ikiwa ni siku ya tatu ya maadhimisho ya Siku ya TAMISEMI.
Amesema fedha hizo zikiwamo shilingi trilioni 1.03 zilizoelekezwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) na shilingi trililioni 1.98 ambazo ni fedha maalumu zilizotumika kujenga mtandao wa barabara za lami katika miji ya kimkakati, Manishaa na Halmashuri za Miji na Jiji la Dar es Salaam.
Amesema hatua hiyo imesaidia kuongezeka kwa mtandano wa barara za lami kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa urefu wa kilomita 699.5 ambayo ni asilimia asilimia 52 kutoka kilomita 1,325.49 mwaka 2015 hadi kufikia kilomita 2,024.99 mwaka 2020.
Amesema kwa upande wa barabara za changarawe kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kulikuwa na barabara zenye urefu wa kilomita 22,089 na baada ya maboresho zimefikia urefu wa kilomita 24,193 ikiwa na ongezeko kwa asilimia 11 huku serikali ikiimarisha barabara za vumbi(udongo) na kufikia urefu wa kilomita 82,428 wakati madaraja makubwa yaliyojengwa ni 99.
“ Mtandao wa barabara zenye hali nzuri na wastani umeongezeka kutoka kilomita 61,798.45 hadi kufikia kilomita 63,164.74 sawa na ongezeko la barabara zenye hali nzuri na wastani urefu wa kilomita 1,366.29, hii inafanya barabara zenye hali nzuri kutoka asilimilia 56 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 58 mwaka huu". Amesma Waziri Jafo na kuongeza;
“Hii inaonesha utashi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhakikisha wananchi wanatengenezewa mtandao wa barabara na hii imesaidia hata wakulima kuweza kusafarisha mazao yao, siku za nyuma watu walikuwa wanateseka sana, tunamshukuru Rais kwa kuwezesha hili".
Akifafanua zaidi anasema mbali na barabara, lakini pia Serikali imewezesha ujenzi wa vituo vya mabasi vya kisasa 24, vituo vya malori, masoko ya kisasa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, madapo ya kisasa katika baadhi ya Miji.
Kuhusu mradi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka katika Jiji la Dar es Salaam (DART), Mhe. Jafo amesema ikiwa kazi za awamu ya pili ya mradi huo ikishika kasi, awamu ya kwanza imekuwa na mafanikio ya kuongeza abiria kutoka watu 75,000 kwa siku hadi kufikia abiria zaidi ya 200,000 kwa siku.
“ Bado tunaendelea na maandalizi ya kumtafuta mtoa huduma wa kudumu atakayekuwa na uwezo kutoa huduma ya mabasi 305 ikilinganishwa na mtoa huduma wa sasa ambaye ana uwezo wa kutoa huduma ya mabasi 140.” Amesema Waziri Jafo
Naye Meneja wa Mfuko wa Barabara, Eliud Nyauhenga amesema magari kuzidisha mzigo ni moja ya changamoto inayorudisha nyuma juhudi za serikali katika maendeleo ya sekta ya barabara.
“ Uzidishaji mizigo kwenye magari kinyume na matakwa ya sheria imekuwa ikichangia sana uharibidu wa barabara, mfano kwa sasa huko vijijini magari yanayokwenda kubeba mazao wamekuwa wakizidisha uzito jambo ambalo linaharibu miundombinu.” Anafafanua Nyauhenga.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa