Wazir wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (Mb) leo Aprili 17, 2020 ametangaza kuongezeka kwa wagonjwa wapya 53 wenye maambukizi ya Virusi vya Corona (Covid 19) ambapo idadi hiyo inafanya wagonjwa wa Covid 19 nchini Tanzania kufikia 147.
Mwalimu amesema wagonjwa wote ni Watanzania katika mikoa ya Dar es Salaam (38), Mwanza (1), Pwani (1), Lindi (1), Kagera (1) na Zanzibar (10) lakini pia amesikitika kutangaza kifo cha mtu mmoja (1) kilichotokana na ugonjwa wa Covid 19.
Waziri Mwalimu amesema tangu tarehe 16 Machi 2020 hadi sasa kuna jumla ya wagonjwa 147 wenye maambukizi ya Virusi vya Corona (Covid 19) nchini, kati yao waliopona ni 11 na vifo 5 vimethibitishwa kutokea.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa