Viongozi wa nchi tatu za Uganda, Comoro na Zimbabwe na wengine wapatao 20 pamoja na mabalozi 83 wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wamethibisha kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais wa Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas (pichani juu) amesema hayo leo tarehe 04 Novemba 2020 alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dodoma.
Dkt. Abbas amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya hafla ya kumuapisha Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, yamekamilika na sherehe hiyo itakayofanyika kesho Novemba 05, 2020 katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Aidha, Dkt. Abbas amesema hafla hiyo itahudhuriwa na viongozi mbalimbali takriban 20 wakiwemo Marais watatu kutoka Uganda, visiwa vya Comoro na Zimbabwe, Makamu ya Rais na Mawaziri Wakuu wa nchi kadhaa wakiwemo pia viongozi wengine mashuhuri kama Rais Mstaafu wa Nigeria Olussegun Obasanjo, Nabii T.B. Joshua, Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, vilevile amesema mabalozi 83 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini watahudhuria pia.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa