Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa leo tarehe 29 Aprili 2020 ametoa taarifa kuwa kuna maambukizi mapya 196 ambayo yote ni ya Watanzania.
Majaliwa amesema kati yao 174 ni wa Tanzania Bara na 22 kutoka Zanzibar ambapo mpaka sasa ya waliopata maambukizi nchini Tanzania ni 480.
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amesema mpaka sasa idadi ya wagonjwa waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 167 (Zanzibar wamepona 36 na Tanzania Bara wamepona 83) ambapo waliofariki ni 16.
Pia, ameeleza kwamba hadi kufikia tarehe 28 Aprili 2020, jumla ya watu 644 wameruhusiwa kutoka Karantini katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Kagera, Songwe, Kigoma, Dodoma na Zanzibar.
Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania kuacha tabia ya kutoa taarifa za uzushi za vifo, kwamba siyo kila kifo kinachotokea kinasababishwa na Ugonjwa wa Corona.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa