Benton Nollo na Bernard Magawa (DMC), Bahi.
Wanawake Mkoani Dodoma wamempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwamba kupitia Serikali ya Awamu ya Tano amewapa kipaumbele akina mama wengi kwa kuwateua katika nafasi mbalimbali za uongozi hali ambayo imewawezesha kushiriki ngazi mbalimbali za maamuzi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda tarehe 8 Machi, 2021 ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ambapo kwa Mkoa wa Dodoma yamefanyika kimkoa wilayani Bahi.
“Tunampongeza sana Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ametuheshimisha sana Wanawake wa Tanzania kwa kutupa kipaumbele katika nafasi mbalimbali za uteuzi akiwemo Makamu wa Rais wa Nchi yetu Mama Samia Suluhu Hassan ambaye anachapa kazi kwa bidii na hajawahi kutuangusha wanawake wenzake.” Amesema Munkunda.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo ambayo huadhimishwa machi 8 kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha usawa kati ya Wanaume na Wanawake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Queen Mlozi amewataka wanawake waliopewa madaraka mbalimbali kuhakikisha wanawashika mkono wanawake wengine ili kwa pamoja washikamane katika kutetea haki za wanawake wenzao.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Josephat Maganga akizungumza kwa niaba ya Wanaume waliohudhuria maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo ‘Wanawake katika uongozi chachu ya kufikia Dunia ya usawa’, amewapongeza wanawake wote walio na nafasi mbalimbali za uongozi kwa jitihada za dhati katika nafasi walizopewa na kuwaasa wanawake wote nchini kusimamia kikamilifu malezi ya watoto wa kike ili kuwaandaa kuwa viongozi wa baadaye.
Awali akiwakaribisha Wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo katika uwanja vya Singidani Bahi mjini, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga amesema wilaya yake imekuwa ya mfano mkoa wa Dodoma katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya serikali hasa utekelezaji wa miradi kwa ufanisi na kumuonyesha matumaini Rais wa Tanzania kwamba hakukosea kuwateua na kwamba wanawake ni waaminifu sana na wakipewa nafasi katika Uongozi wanawajibika ipasavyo.
Picha na Matukio:
Maandamano yakipita mbele ya Mgeni Rasmi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi akiwasalimia Wanawake na wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yamefanyika wilayani Bahi kimkoa tarehe 08 Machi 2021.
Waheshimiwa Madiwani Wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yamefanyika wilayani Bahi kimkoa tarehe 08 Machi 2021.
Katibu Mkuu Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Queen Mlozi (aliyevaa kilemba cha bluu) akimkabidhi Kiti Mwendo (wheel chair) Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Phillipina Philipo (kulia) kilichotolewa na na Karakana ya Walemavu Dodoma (KAWADO) ili itumike katika Hospitali ya Wilaya ya Bahi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yamefanyika wilayani Bahi kimkoa tarehe 08 Machi 2021. Pamoja na kiti hicho pia, KAWADO wametoa kiti kingine kimoja kwa Mwanafunzi Mwenye Ulemavu, Brian Msendekwa wa Shule ya Msingi Mphangwe na Baiskeli moja ya magurudumu matatu kwa Mwanafunzi Mwenye Ulemavu, Vaileti Maloda wa Shule ya Msingi Lamaiti. Anayeshuhudia katikati ni Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda.
Picha za juu ni Katibu Mkuu Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Queen Mlozi (kushoto) pamoja na viongozi mbalimbali wakikabidhi msaada wa nguo zilizokusanywa na Tasisi ya Vijana ya Active Hope kutoka kwa watu mbalimbali wenye uwezo kwa ajili ya kuwapatia wahitaji, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yamefanyika wilayani Bahi kimkoa tarehe 08 Machi 2021.
Wananchi mbalimbali wamejitokeza kuchangia damu ili kuwasaidia akina mama na watoto wenye uhitaji, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yamefanyika wilayani Bahi kimkoa tarehe 08 Machi 2021.
Baadhi ya akina mama wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yamefanyika wilayani Bahi kimkoa tarehe 08 Machi 2021.
Walimu Wanawake wa Shule ya Msingi Bahi Misheni na Shule ya Sekondari Bahi wakiimba shairi maalum wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yamefanyika wilayani Bahi kimkoa tarehe 08 Machi 2021.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba (kulia) akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Pius Mwaluko (kushoto) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yamefanyika wilayani Bahi kimkoa tarehe 08 Machi 2021. (Picha zote na Benton Nollo).
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa