Benton Nollo, Bahi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma Mganga amewapa Ilani ya siku 30 wananchi wote waliopewa viwanja katika Mji wa Bahi “Kitalu J” kuhakikisha kuwa wanalipa fedha zote wanazodaiwa kabla siku hizo 30 kuisha yaani kuanzia tarehe 30 Januari, 2019 hadi tarehe 28 Februari, 2019.
Mganga ameitoa ilani hiyo ofisini kwake tarehe 07 Februari, 2019 na kusisitiza kwamba mpaka kufikia tarehe 28 Februari, 2019 yeyote ambaye atakuwa hajalipia kiwanja chake basi kiwanja hicho atapatiwa mtu mwingine bila taarifa na hatakuwa na haki tena juu ya kiwanja hicho.
“Napenda niwaarifu wananchi wote waliopatiwa viwanja katika Mji wa Bahi hasa “Kitalu J” kuwa ilani hii ni ya siku 30, hivyo ikifika tarehe 28 Februari mwaka huu (2019) mwananchi yeyote ambaye atakuwa bado hajalipia kiwanja anachodaiwa basi atambue kuwa kiwanja chake atapatiwa mtu mwingine tena bila yeye kutaarifiwa na hatakuwa na haki tena juu ya kiwanja hicho”. Alisema Mganga.
Mganga alifafanua kuwa wahusika wote watambue kwamba kwa wao kutolipia viwanja hivyo, wanaikosesha Serikali Mapato kwani kupitia mapato hayo Serikali inapata fursa ya kuboresha huduma mbalimbali kwa wananchi.
Aidha, katika Ilani hiyo Mganga amewataka wahusika wote kulipa maduhuli hayo kwa wakati na kabla ya kufanya hivyo wawasiliane na Ofisi ya Ardhi na Ofisi ya Mweka Hazina katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ili wapatiwe bili ya malipo na kusisitiza kuwa malipo yote yanatakiwa kufanyika Benki na ofisi haitahusika na malipo yoyote ya fedha taslimu.
Pamoja na Ilani hiyo, Mganga aliweka wazi orodha nzima ya wadaiwa hao na kuelekeza kuwa ibandikwe kwenye mbao za matangazo ikiwa inaainisha namba na ukubwa wa kiwanja kwa kila muhusika.
Kupata orodha na majina ya wadaiwa, Bofya hapa http://www.bahidc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/orodha-ya-wasiolipia-viwanja-katika-mji-wa-bahi-kitalu-j-hii-hapa.pdf
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa