Benton Nollo na Alinikyisa Humbo
Watendaji wa Kata na Vijiji wilayani Bahi wamepongezwa kwa kusimamia vema ukusanyaji wa mapato baada ya kuvuka malengo ya makusanyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatuma R. Mganga kwa Watendaji wa Kata 20 kati ya Kata 22 na Watendaji wa Vijiji 45 kati ya vijiji 59 wilayani humo kwa kukusanya mapato ya vibali vya mifugo kwa zaidi ya asilimia 80 ya malengo waliyokuwa wamewekewa kwa mwaka huo.
Dkt. Mganga ameyasema hayo Julai 15, 2019 katika kikao kazi alichokiitisha cha Watendaji wa Kata na Watendaji wa Vijiji kwa lengo la kufanya tathmini ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na kupeana malengo mapya kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Akizungumza na Watendaji hao, Dkt. Mganga amesema kuwa anawapongeza sana Watendaji wote waliofikia lengo na wengine kuvuka lengo katika suala zima la ukusanyaji wa mapato hasa ya vibali vya mifugo.
Dkt. Mganga amesema Watendaji wote waliofanya vizuri kwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao watatunukiwa vyeti maalum vya kutambua juhudi zao katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi ili kurahisisha zaidi ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
“Kata zote zilizofanya vizuri na zilizovuka malengo ya makusanyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019, Watendaji husika watapatiwa motisha na Halmashauri pamoja na vyeti maalum ikiwa ni kutambua mchango wao katika kukusanya mapato ya serikali na kwa wale waliofanya vibaya nao watapatiwa stahili yao”. Alisema Dkt. Mganga.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa malengo ya makusanyo ya mapato ya vibali vya mifugo kwa kila kata na kijiji, Kaimu Mweka Hazina wa wilaya hiyo Arbogast Chrisant alizitaja kata 20 zilizofanya vizuri ,ambazo ni Chikola,Chipanga, Msisi, Ibihwa, Ilindi, Nondwa, Mtitaa, Bahi, Kigwe na Lamaiti. Kata nyingine Chali,Makanda, Mpalanga, Mundemu, Chifutuka, Chibelela, Mwitikira, Mpinga, Zanka na Babayu. Hata hivyo, Chrisant alisema kata 2 za Mpamantwa na Ibugule hazikufikisha malengo.
Aidha, kwa upande wa vijiji vilivyofanya vizuri Chrisant alivitaja kuwa ni Chikola ,Tinai, Magaga, Chipanga “B”, Nkulughano, Chimendeli, Nchinila, Mnkola, Msisi, Nagulo Bahi, Chiguluka, Chipanga “A” na Bahi Makulu. Vijiji vingine ni Mindola, Chidilo, Chali Igongo, Zejele, Mundemu, Nondwa, Ilindi, Chali Makulu, Kisima cha Ndege, Chikopelo , Lamaiti, Kigwe, Zanka, Bankolo, Chonde, Mpalanga, Bahi Sokon,.Msisi, Chibelela, Kigwe, Makanda, Mpinga, Mtitaa, Babayu, Lamait, Bahi, Mwitikira, na M Mundemu, hata hivyo Chrisant alivitaja vijiji ambavyo havikukusanya mapato kufikia asilimia 50% kuwa ni vijiji 14 ambavyo ni Ikumbulu, Chibelela, Mayamaya , c Chifutuka, Nkhome, Asanje, Mzogole, m Mpamantwa, Mkondai, Mapanga, Chali Isanga, Ibugule, Nholi, na kijiji cha Mkakatika.
Akijibu taarifa hiyo Dkt Mganga ameseama kuwa Kata na Vijiji vilivyofanya vizuri vitapewa zawadi ya vyeti na pia aliwataka Watendaji wa Vijiji na Kata ambazo hazikuweza kufikia lengo kuendelea kutafuta mbinu mbadala ya kuweza kukusnya mapato hiyo ili kuweza kutimiza lengo la Serikali katika ukusanyaji wa mapato mbalimbali ya Serikali .
Dkt Mganga amesema kuwa miongoni mwa Kata zilizofanya vizuri Kata tatu bora zitapewa zawadi lakini pia alisistiza kuwa Kata mbili ambazo hazikufanya vizuri zitawajibishwa
Mbali na taarifa ya mapato Dkt Mganga alizungumzia suala la uadilifu na nidhamu katika kazi alisema kuwa kiongozi yeyote anayejitambua hata utendaji wake wa kazi unakuwa bora na wenye uadilifu wa hali ya juu lakini pia alitoa rai kwa Watendaji wa Kata na Vijiji kuwa waadilifu katika majukumu waliopewa ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika kufanya na kutimiza wajibu wa Serikali
“Hii Halmashauri ni yetu sote basi tukipewa majukumu tufanye kwa uadilifu na tutimize malengo na majukumu mbalimbali ambayo tumepewa na Serikali pia tuheshimiane na kufuta taratibu zote za kikazi hakuna kinachoshindikana vyote vinawezekana tukizingatia uadilifu katika kazi”alisema Dkt Mganga.
Na katika kuendelea kusisistiza suala la uadilifu kazini Kaimu Afisa utumishi, Chrispine Katalyeba amewataka watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kwamaba kila mmoja afuate utaratibu uliopokulingana sheria ya kazi,pia aliwataka kuzingatia sheria ya mavazi katika utumishi wa umma,laini pia aliwaasa kuepuka kupokea au kutoa rushwa kwani nikosa kisheria.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa