Na Benton Nollo, Mkakatika
Wenyeviti wa Vijiji wilayani Bahi wameagizwa kuzisimamia Shule Shikizi katika maeneo yao ili ziweze kuleta matokeo chanya kwa jamii husika.
Hayo ya mesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda alipotembelea Shule Shikizi ya Lowassa inayohudumia vitongoji vya Nkomango na Mlingeni katikaKijiji cha Mkakatika, Kata ya Mpamantwa wilayani humo tarehe 09 Januari 2020.
Munkunda amesema kuwa Wenyeviti wa Vijiji wanapaswa kutambua kuwa shule zote shikizikatika maeneo yao ni mali ya wananchi hivyo wao kama viongozi katika maeneo yaowana wajibu wa kuzisimamia ipasavyo katika uendeshaji wake na wajibu waSerikali ni kupeleka walimu na pale inapotokea changamoto ya ukosefu wa walimubasi kijiji kina wajibu wa kumtafuta mwalimu wa kujitolea ili awafundishewanafunzi.
Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa Wenyeviti wa Vijiji wahakikishe kuwa wanashirikiana na wananchi katika maeneo hayo kuboresha mazingira ya wananfunzi kujifunzia iliwatoto wanapotoka nyumbani kwao wavutiwe kusoma katika shule hizo kwa uwepo wa mandhari nzuri.
“Kama kweli tunaunga mkono jitihada za Serikali yetu katika kuboresha sekta ya elimu,basi sisi kama viongozi tutambue kuwa tunawajibu wa kuwahamasisha wananchi kuboresha miundombinu ya shule hizi shikizi hivyo mambo yote yaliyo chini yauwezo wetu pamoja na wananchi tunayatimiza”. Amesema Munkunda na kuongeza.
“Mwenyekiti na kuagiza na agizo hili nalitoa kwa Wenyeviti wa Vijiji wote ambao wanazo Shule Shikizi kwa mpaka kufikia tarehe 09 Machi 2020 mazingira ya shule hizo katika maeneo yao yawe yameboreshwa vinginevyo wananchi hawakuwa na uhitaji wakuanzisha shule hizo”.
Munkunda amesema kuwa ametoa muda mrefu ili Wenyeviti wa Vijiji wawajibike ipasavyo kuwasimamia wananchi na katika zoezi hilo pia amewaagiza kuainisha vema mipakaya shule hizo kwa kuweka alama za kudumu.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkakatika Remy Juma amemhakikishia Mkuu waWilaya hiyo kuwa atalisimamia na kulitekeleza kikamilifu agizo lake.
Naye Nyambuya Machela ambaye ni moja ya wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo amemueleza Mkuu wa Wilaya kuwa kuanzishwa kwa shule hiyo kwao kumekuwa namanufaa makubwa kwa sababu Shule ya Msingi Mkakatika ipo umbali wa takriban kilomita 10.
Hivyo,watoto wanapofikia umri wa kuanza shule wazazi huingiwa na hofu kuhusu usalamawao wanapotoka nyumbani kwenda shule na kurudi.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ambaye aliambatana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzina Usalama ya Wilaya ya Bahi, Msimamizi wa shule hiyo Abdul Juma Kivuma alitoataarifa kwamba shule hiyo ina wanafunzi 107 ambapo Darasa la Awali ni 26,Darasa la Kwanza 48 na Darasa la Pili 33.
Shule Shikizi ambazo mpaka sasa zimetembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi ni Lioni ya Kijiji cha Bahi Sokoni, Suguta ya Kijiji cha Bahi Makulu, Mpamantwa Kijiji cha Mpamantwa na Nyerere ya Kijiji cha Ibihwa.
Picha na Matukio:
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akizungumza na Viongozi pamoja na baadhi wa wazazi wa Kitongoji cha Nkomango, Kijiji cha Mkakatika alipotembea Shule Shikizi ya Lowassa tarehe 09 Januari 2020.
Mwalimu Abdul Juma Kivuma ambaye ni Msimamizi wa Shule Shikizi ya Lowassa iliyopo Kijiji cha Mkakatika, akisisitiza jambo wakati akitoa taarifa ya shule hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi (hayupo pichani), wakati wa ziara yake aliyoifanya shuleni hapo tarehe 09 Januari 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akifurahi pamoja na Wanafunzi wa Shule Shikizi ya Lowassa iliyopo Kijiji cha Mkakatika alipotembea Shule hiyo tarehe 09 Januari 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akiimba wimbo pamoja na Wanafunzi wa Shule Shikizi ya Lowassa iliyopo Kijiji cha Mkakatika alipotembea Shule hiyo tarehe 09 Januari 2020.
SGT Dankan Mbughi (kulia) akiwafundisha gwaride wanafunzi wa Shule Shikizi ya Lowassa iliyopo Kijiji cha Mkakatika alipotembea Shule hiyo tarehe 09 Januari 2020.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Bahi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo (hayupo pichani), wakati wa ziara yake aliyoifanya katika Shule Shikizi ya Lowassa iliyopo Kijiji cha Mkakatika tarehe 09 Januari 2020.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkakatika, Remmy Juma akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Bahi (hayupo pichani), wakati wa ziara ya mkuu huyo wa wilaya alipotembelea Shule Shikizi ya Lowassa iliyopo kijijini hapo tarehe 09 Januari 2020.
Baadhi ya wazazi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Bahi (hayupo pichani), wakati wa ziara yake aliyoifanya katika Shule Shikizi ya Lowassa iliyopo Kitongoji cha Nkomango katika Kijiji cha Mkakatika tarehe 09 Januari 2020. (Picha zote na Benton Nollo).
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa