Mhe. Rosemary Senyamule (Mkuu wa Mkoa wa Dodoma) Leo Januari 28/01 /2025 amefanya Ziara na kukagua Miradi inayotekelezwa katika Wilaya ya Bahi ambapo alikagua ujenzi wa Madarasa Matatu(3) katika shule ya Msingi Kusila katika kata ya Mtitaa na kukagua ujenzi wa bweni la Wasichana katika shule ya Sekondari Mwitikira.
Aidha, katika Ziara hiyo ambayo aliongozana na
Katibu Tawala wa Wilaya Ndugu. Mwanamvua Bakari Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi. Zaina M. Mlawa na timu ya Wataalamu wa Halimashauri ambapo kwa pamoja walishiriki upandaji miti nakupanda Miti minne(4), miti maji mitatu(3) na Mti wa Mzambarau mmoja (1) katika bweni hilo, baadaye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alifanya Mkutano wa hadhara katika shule ya Sekondari Mwitikira kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitatua, Katika mkutano Mhe. Senyamule alisisitiza jamii ya watu wa Bahi kuwekeza zaidi katika elimu.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa