Benton Nollo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefariki dunia kwa tatizo la moyo la mfumo wa umeme katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ameutangazia umma kutokea kwa kifo cha kiongozi huyo wa juu nchini akiwa jijini Tanga.
“Tumempoteza kiongozi wetu shupavu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alilazwa tarehe 06 Machi mwaka huu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo la mfumo wa umeme ambalo alikuwa nalo kwa zaidi ya miaka 10.” Amesema Mama Samia Suluhu Hasssan.
Rais Dkt. Magufuli alilazwa tarehe 06 Machi 2021 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kuruhusiwa Machi 07, 2021 na kuendelea na majukumu na tarehe 14 Machi 2021 alijisikia vibaya na kupelekwa Hospitali ya Mzena ambako alitibiwa mpaka umauti ulipomkuta jana tarehe 17 Machi 2021 majira ya saa 12 jioni.
Makamu wa Rais ametangaza kuwa nchi yetu Tanzania itakuwa na maombolezo ya siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli enzi za uhai wake.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa