Leo Tarehe 10 May,2025 Imefanyika hafla ya kuwapongeza Walimu na Shule zilizofanya vizuri kitaifa na kimkoa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.
Ikiwa ni kawaida kwa Uongozi Wa Wilaya hiyo Kutoa motisha kwa kutoa Tuzo na fedha tasilimu kwa Shule,walimu, wanafunzi na wazazi ambao ambao kwa pamoja kama wadau wanachangia kila mtu kwa nafasi yake kuhakikisha suala la elimu kwa ngazi zote linafanyika kwa mafanikio.
Katika hafla hiyo ambayo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Joachim Thobias Nyingo ambapo na wadau mbalimbali wa elimu walialikwa kushuhudia utoaji wa Tuzo hizo katika Wilaya hiyo.
Ikumbukwe kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Bahi imeshika nafasi ya Pili kitaifa katika matokeo ya elimu Msingi ikiwa ni muendelezo Wa kuvunja rekodi yake ya matokeo yaliyopita ambapo Wilaya hiyo ilishika nafasi ya Tatu kitaifa.
Uongozi Wa Wilaya ya Bahi kwa maana ya timu ya Halmashauri ya Wilaya inayojumuisha wakuu wa Divisheni mbalimbali na vitengo chini Mkurugenzi Mtendaji Bi.Zaina Mlawa kwa kushirikiana na timu ya Madiwani chini Mhe.Donald Mejetii Pamoja timu ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mhe.Joachim Thobias Nyingo na Katibu Tawala wa Bahi Bi.Mwanamvua Bakari wameendelea kushirikiana katika kuhakikisha adhma ya Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Wananchi wanapata elimu Bora bila kujali utofauti Wao kiuchumi inatimia.
Aidha,Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe.Keneth Nollo amewaomba wananchi wa Bahi kumrejesha tena Mhe.Rais wa Jamhuri ya Mhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi wa Oktoba 2025 kwa kwenda kujiandikisha katika awamu ya pili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ambao utaanza rasmi tarehe 16 May mpaka 22 May,2025 ili akamilishe Miradi ya maendeleo na kukuza uchumi wa Nchi kwa ujumla.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa