Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ametoa wito wa kutumia maarifa yanayopatikana katika maonesho ya Nanenane mwaka 2020 ili kuleta mabadiliko yenye tija katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.
Kauli hiyo aliitoa wakati akifungua maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati yanayoendelea katika uwanja wa Nanenane Nzuguni jijini Dodoma.
“Tuna kila sababu ya kujitathmini, maonesho haya yanafanyika kila mwaka, bado tuna fursa kubwa tulizokuwa nazo ila hatujatumia vya kutosha fursa hizi. Leo ukienda Kongwa, Mpwapwa, Manyoni, Itigi, Mkalama, Bahi, mimi imani yangu kama mafunzo yanayotolewa hapa yakitumika kwa asilimia 75 tutapata mafanikio makubwa sana katika uchumi wetu. Imani yangu bado maarifa hayajatumika kwa asilimia kubwa”. Amesema Waziri Jafo na kuongeza;
"Maarifa hayo yakifanyiwa kazi katika miaka mitano ijayo itaifanya nchi kuingia katika uchumi wa kati uliyoendelea kuimarika zaidi".
Waziri Jafo amesema kuwa maarifa hayo yanatakiwa kupelekwa katika utendaji zaidi kutoka katika dhana ya maonesho na kwenda katika dhana ya utekelezaji kivitendo.
“Lakini fahamu nchi yetu tupo katika eneo la kimkakati kijiografia. Ni miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, tupo ukanda wa SADC, tunafursa ya kujenga uchumi wetu kupitia kilimo, mifugo na uvuvi”. Mmesema Jafo.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa